HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 4, 2023

Shilingi ML 200 kutumika mradi wa maji Longido

 

Meryprisca Mahundi Naibu Waziri wa maji akizungumza na wananchi wa Longido.

Meryprisca Mahundi Naibu Waziri wa maji akipokelewa na Wananchi wa Longido.
Mhandisi Justine Rujomba Mkurugenzi wa AUWSA akisoma taarifa ya mradi wa Maji wa Wilaya ya Longido mbele ya naibu Waziri wa maji.

Na Jane Edward, Arusha
NAIBU Waziri wa maji Meryprisca Mahundi amesema serikali itaharakisha kuleta fedha zaidi ya Milioni 200 kwaajili ya mradi wa Maji ambayo umekelezwa ili kupunguza changamoto inayowakabili Wananchi wa kata Sinya Wilaya Longido Mkoani Arusha ambao wamekuwa wakipata adha ya kufata Maji umbali wa zaidi ya kilometa 10.

Akizungumza na wananchi katika kata hiyo wakati akiwa katika ziara yake ya kutembelea maendeleo ya miradi ya maji inayotekelezwa na wizara ya maji kupitia mamlaka ya maji jiji la Arusha (Auwsa)pamoja na Ruwasa.

Naibu Waziri huyo amesema katika kata ya Sinya jambo la kwanza ni kuhakikisha maji yanapatikana kwa haraka ili kuunga sera ya Rais Samia ya kumtua Mama Kichwani.

"Visima vinavyohitajika katika kijiji hiko ni kumi na nane na kwamba milioni 200 zitakazo kuja zitapunguza changamoto hiyo kwani serikali inataka kila kata na kila kijiji kupata maji kwa haraka na ya uhakika na sisi kama wizara tuko hapa kuhakikisha tunasimamia jambo hilo"Alisema Meryprisca

Awali akisoma taarifa ya mradi wa maji Wilaya Longido na Namangakirugenzi wa mamlaka ya maji safi na usimamizi wa mazingira (AUWSA)Justine Rujomba anasema Kanda ya Longido ni moja ya ofisi za kanda za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA) inayotoa huduma ya majisafi katika Mji wa Longido, Kata ya Namanga na baadhi ya maeneo katika kata ya Kimokouwa ambapo Chanzo pekee cha maji kwa sasa ni mto Simba uliopo Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.

"kulingana na uwezo wa chanzo cha mto simba, maji yanayozalishwa kwa sasa ni wastani wa lita 719,000 hadi lita 1,500,000 kwa siku ambayo hayatoshelezi mahitaji ya jumla ya lita 3,918,000 kwa siku (mji wa Longido lita 1,527,000 kwa siku na kata za Kimokouwa na Namanga ni lita 2,391,000 kwa siku) ambapo kata hizo hazikuwepo kwenye usanifu wa mradi wa maji Longido"Alisema Mhandisi Rujomba.

Aidha alisema idadi ya wananchi katika eneo la huduma inakadiriwa kufikia 49,000 ambapo Mamlaka ya Maji (AUWSA) imefanikiwa kuongeza mtandao wa usambazaji wa majisafi

hadi kufikia km 187.67 baada ya utekelezaji wa mradi wa majisafi Longido kuelekea Namanga kukamilika.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Longido Steven Kiruswa akizungumza kwa niaba ya wananchi wake ameishukuru wizara ya Maji kwa kuwakumbuka wananchi wake katika upatikanaji wa Maji na kwamba watahakikisha miundombinu ya maji inalindwa ili isiharibike.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad