Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umewaalika wanachama na wananchi kwa ujumla kutembelea banda la Mfuko huo wakati huu wa Maonesho ya Nanenane mwaka 2023 yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wananchama, PSSSF, Bw. James Mlowe amesema pamoja na mambo mengine Mfuko una maslahi mapana katika maonesho hayo hasa ikizingatiwa ni mdau mkubwa katika masuala ya kilimo na ufugaji.
Alisema, Mwanachama akifika kwenye banda la Mfuko atapata Taarifa za Michango yake, Taarifa za Mafao yatolewayo na Mfuko, Taarifa kuhusu Uwekezaji unaotekelezwa na Mfuko lakini pia wote watakaofika kwenye banda hilo watapata elimu ya Hifadhi ya Jamii.
"PSSSF tunawahakikishia wanachama, wakiwemo wastaafu kuwa wakifika kwenye banda letu watapatiwa huduma sawia kama zile zinazotolewa kwenye ofisi zetu zilizoenea nchi nzimTanzania Bara na Tanzania Zanzibar." Alifafanua Bw. Mlowe.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera, mataifa 30 yalithibitisha kushiriki katika maonesho hayo yaliyobeba kauli mbiu isemayo "Vijana na Wanawake ni msingi imara wa mfumo endelevu wa chakula".
"Mfumo endelevu wa chakula utajenga nguvu kazi imara, na hatimaye itapelekea ajira kwenye sekata binafsi na umma ambayo sisi tunaihudumia, hivyo kwetu sisi maonesho haya yana maana kubwa sana kwetu." Alibainisha Bw. Mlowe.
Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,Bw. Ramadhani Mgaya akimkabidhi Bw. Julius Mlwafu wa UTT Mbeya alipotembelea banda la PSSSF katika maadhimisho ya Nanenane yanayoendelea katika katika viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya.
Afisa wa Mfuko, Irene Museti (kushoto) akimhudumia mteja aliyetembelea banda la PSSSF katika maonesho ya Nanenane yaliyianza rasmi leo Agosti 1, 2023, katika viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya.Kikosi kazi cha timu ya PSSSF kilichoweka "Kambi" viwanja vya John Mwakangale tayari kuwahudumia wananchama na kutoa Elimu kwa Umma kuhusu Hifadhi ya Jamii.
No comments:
Post a Comment