HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 29, 2023

NBAA YATOA WARSHA KWA NJIA YA MTANDAO KWA WANAFUNZI WANAOTEGEMEA KUFANYA MITIHANI YA BODI

 


Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (​NBAA) imeendesha warsha kwa njia ya mtandao kwa wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi ili kuongeza ufanisi kipindi wanapokwenda kufanya mitihani hiyo.

Akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno amesema kwa mara ya kwanza wamefanya warsha  hiyo kwa njia ya mtandao na kuwakutanisha wanafunzi wa ngazi mbalimbali wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi katika ngazi mbalimbali ikiwa na lengo la kuwanoa kwenye mbinu mbalimbali za mitihani hasa kwenye maeneo yanayokuwa na changamoto kwa watahiniwa wa Bodi.

CPA Maneno amesema yapo Masomo yanaleta changamoto na kiwango cha ufaulu unakuwa mdogo hivyo tumewaletea walimu wa Masomo hayo kutoka vyuo na Taasisi mbalimbali ili waweze kuwapa uzoefu na  mbinu mbalimbali za kuweza kujiandaa na kufanya mitihani ya Bodi.

"Tumewasisitiza sana namna ya kujiandaa wasijiandae kiholelaholela bali waweke muda wa kutosha kwenye kujifunza kwani kuna tofauti kubwa sana kati ya watahiniwa wa vyuo na watahiniwa wa mitihani ya Bodi " alisema CPA Maneno

Pia amesema lengo kubwa la NBAA ni kuona wanapandisha kiwango cha ufaulu kwa mitihani mbalimbali pamoja na kuongeza kiwango cha uelewa ili kipindi wanapomaliza mitihani yao waweze kuwa wabobezi kwenye masuala ya Uhasibu na Ukaguzi.

Naye Meneja wa Idara ya Elimu na Mafunzo NBAA, Peter Lyimo anasema Bodi hiyo  imejipanga vizuri ili kuhakikisha kila mtahiniwa anafanya mitihani  vizuri na kuhakiksiha wanaondoa changamoto zote.
Meneja wa Huduma za Shirika (NBAA) CPA Kulwa Malendeja akiwakaribisha wakufunzi waliofika kwa ajili ya kutoa mafunzo  katika warsha  iliyoandaliwa na NBAA kwa njia ya mtandao kwa wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi.
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akiwakaribisha wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani mbalimbali ya Bodi ambao walikuwa wakisikiliza Warsha hiyo kwa njia ya mtandao.
Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, CPA Dkt. Emmanuel Christopher akitoa  elimu kuhusu namna ya kujiandaa na kufanya masomo ya B1 na C3 kwa wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi waliokuwa wanafuatilia kwa njia mtandao.
Mkufunzi CPA Rashid Mganwa akitoa  elimu kuhusu namna ya kujiandaa  na kufanya masomo ya B2 na C1 kwa wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi waliokuwa wanafuatilia kwa njia mtandao.
Mkufunzi CPA Nicholas Massawe akitoa elimu kuhusu mabadiliko ya masomo ya Kodi yaani B4 na C4  kwa wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi waliokuwa wanafuatilia kwa njia mtandao mafunzo hayo.
Mkufunzi CPA Ansbert Kishamba akitoa  elimu kuhusu namna ya kujiandaa na kufanya somo la B5  kwa wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi.
CPA Douglas Munah akitoa elimu kuhusu vitu mbalimbali anavyozingatia mtungaji wa mitihani ya Bodi.
Meneja wa Idara ya Elimu na Mafunzo NBAA, Peter Lyimo akijibu maswali ya washiriki wa warsha kwa njia ya mtandaoni .

1 comment:

  1. Well done NBAA. The digital channels and digital modus operandi are the only ways to survive in the future of the profession. Let us keep it up.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad