HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 24, 2023

SERIKALI YAANZA MAPITIO YA SERA YA WATU WENYE ULEMAVU

 

Na Mwandishi Wetu, DODOMA

OFISI ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imeanza kufanya tathmini na mchakato wa mapitio ya Sera ya Maendeleo na Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2004 ili kukidhi mahitaji ya sasa.

Akifungua kikao cha wadau Agosti 24, 2023 jijini Dodoma cha kupitia taarifa ya awali ya mapitio hayo, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Prof.Jamal Katundu, amesema mapitio hayo yanafanywa na serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake(UN WOMEN) huku akitaka yazingatie uwakilishi wa makundi yote ya Watu wenye Ulemavu ili kuwa na sera bora.

Naye, Mwakilishi wa UN WOMEN, Jacob Kayombo, amesema shirika limeridhishwa na hatua iliyofikiwa ya mchakato huo na kwamba wanaamini itakamilika kwa wakati.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA), Jonas Lubago, ameishukuru serikali kwa kutimiza ahadi ya kufanya maboresho ya sera hiyo na kuahidi kushiriki kikamilifu ili kuwa na maboresho mazuri ya sera.

Awali, Mshauri Elekezi ambaye ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt. Consolata Sulley, amesema katika hatua ya awali ya mapitio utafanyika utafiti kwa kupata maoni kutoka kwa wadau ili kuwa na sera bora inayozingatia haki na masuala ya kijinsia kwa Watu wenye Ulemavu.



Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu akizungumza na wadau wakati wa kikao kazi cha kupitia taarifa ya awali ya mapitio ya Sera ya Maendeleo na Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2004, kilichofanyika katika Ofisi ya WCF, Kambarage Tower, Jijini Dodoma leo tarehe 24 Agosti, 2023.Baadhi ya wadau wakifuatilia kwa maelezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha kupitia taarifa ya awali ya mapitio ya Sera ya Maendeleo na Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2004, Jijini Dodoma tarehe 24 Agosti, 2023.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Said Mabie akieleza jambo wakati wa kikao kazi hicho.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Watu wenye Ulemavu, Jacob Mwinula (kushoto) akifafanua jambo wakati wa wakati wa kikao kazi cha kupitia taarifa ya awali ya mapitio ya Sera ya Maendeleo na Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2004, kilichofanyika katika Ofisi ya WCF, Kambarage Tower, Jijini Dodoma leo tarehe 24 Agosti, 2023. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango, Godfrey Chambo.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake (UN WOMEN), Jacob Kayombo akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Mshauri Elekezi ambaye ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam(UDSM), Dkt. Consolata Sulley akiwasilisha taarifa ya awali ya mapitio ya Sera ya Maendeleo na Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2004, wakati wa kikao kazi hicho kilichofanyika katika Ofisi ya WCF, Kambarage Tower, Jijini Dodoma leo tarehe 24 Agosti, 2023.Wadau waifuatilia taarifa ya awali ya mapitio ya Sera ya Maendeleo na Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2004, wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi ya WCF, Kambarage Tower, Jijini Dodoma leo tarehe 24 Agosti, 2023.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA), Jonas Lubago akieleza jambo wakati wa kikao kazi hicho.

Mhadhiri Msaidizi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, Upendo Komba akichangia jambo wakati wa kikao kazi hicho.



Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu (katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mara baada ya kufungua rasmi kikao kazi cha kupitia taarifa ya awali ya mapitio ya Sera ya Maendeleo na Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2004, kilichofanyika katika Ofisi ya WCF, Kambarage Tower, Jijini Dodoma leo tarehe 24 Agosti, 2023. 
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad