Na Alex Siriyako, TMC Tabora
MKURUGENZI wa Manispaa ya Tabora Elias Mahwago Kayandabila
amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha Sh.Bilioni 1.2 kwa
ajili ya miundombinu ya elimu kwa wanafunzi wa kidato cha tano kwa
shule za Sekondari Milambo na Kazima.
Kayandabila ametoa
shukrani zake za dhati kwa Rais leo Agosti 15, 2023 baada ya kutembelea
shule hizo katika kuhakikisha utekelezaji wa maagizo ya Serikali ya
kuzitaka shule zote za Sekondari zenye kidato cha tano kuhakikisha kuwa
zinawapokea wanafunzi wa kidato cha tano kuanzia leo.
"Ikumbukwe
kuwa, wanafunzi wa kidato cha tano kwa shule nyingi nchini wamepokelewa
katika miundombinu mipya kabisa na ya kisasa mathalani Mabweni, Madarasa
pamoja na Vyoo. Shule ya Sekondari Milambo ni miongoni mwa shule kongwe
kabisa nchini.
" Na haijapata ujenzi mkubwa wa Miundombinu
mipya kama huu wa awamu hii wa mabweni manne, madarasa manne na matundu
kumi ya vyoo.
"Pia Shule ya Sekondari Kazima ikiwa nayo ni
miongoni mwa shule kongwe imepata fursa ya ujenzi mkubwa wa miundombinu
mipya ya kisasa kwa maana ya mabweni matatu, madarasa manne pamoja na
matundu 10 ya vyoo."
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Mirambo
Mwalimu Daudi Mapere ameishukuru sana serikali ya awamu ya sita
inayoongozwa na Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia shule yake Sh.milioni
670 kwaajili ya ujenzi wa mabweni manne, madarasa manne pamoja na
matundu 10 ya vyoo na ameahidi matokeo makubwa kwasababu miundombinu
imekuwa mizuri sana.
Wakati huo huo Mwalimu Elizabethi Masanja,
ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Kazima amemshukuru Rais kwa
kuwaondolea adha ambayo wangeipata kama wangepokea ongezeko hili la
wanafunzi bila maboresho haya ya Miundombinu.
Mwalimu Masanja
amefafanua awali Shule ya Kazima ilikuwa inapokea wanafunzi 200 wa
kidato cha tano , na kwa mwaka huu inatarajia kupokea wanafunzi 546
Hivyo
bila maamuzi magumu, makubwa, na kuungwa mkono ya serikali koboresha
miundombinu, watoto hawa wangesomea mazingira ya shida sana. Hivyo
amesishukuru Serikali kwa kusimamia vyema sana Ilani ya Chama Cha
Mapinduzi(CCM)hususani kwenye sekta ya elimu.
Kwa
upande wao wanafunzi wa Kazima Sekondari na Mirambo kwa awamu tofauti
tofauti wamemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na
kuwajengea miundombinu bora ya elimu na wameahidi kufanya vizuri katika
mitihani yao.
MKURUGENZI wa Manispaa ya Tabora Elias Mahwago Kayandabila akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Kazima,kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Kazima, Mwalimu Elizabethi Masanja
MKURUGENZI wa Manispaa ya Tabora Elias Mahwago Kayandabila akisalimiana na mmoja wa Wanafunzi shule ya Sekondari Milambo mara baada kuwapokea wanafunzi hao wa kidato cha tano kwenye mabweni mapya yaliyojengwa kwenye hiyo kwa fedha za Serikali kuu.Pichani kulia kwake alieambatana nae ni Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari - TMC Mwalimu Nyahori Mang'ari
No comments:
Post a Comment