Na Mwandishi Wetu.
MASHINDANO ya wazi ya mchezo wa Pool ambayo hufanyika kila mwaka katika kipindi cha siku kuu ya nanenane yameaanza rasmi leo katika Hoteli ya Nefaland Manzese jijini Dar es Salaam yajulikanayo kama “88” Grand Open Pool Competitions 2023..
Akizungumza na Waandishi wa habari Mratibu wa Mashindano hayo na Mwakilishi wa Kampuni ya Watengenezaji wa meza za Pool ya Kenice, Michael Machela alisema mashindano hayo yatachukua siku tatu yakijumuisha timu za Mikoa ,mchezaji mmoja mmoja Wanaume pamoja na Wanawake.
Alisema Machela, jumla ya timu 16 zilijiandikisha na tayari zinashiriki mashindano hayo.
Machela pia alisema jumla ya wachezaji 128 wamethibitisha kushiriki na tayari wamesharipoti eneo la mashindano ikiwa ni pamoja na Wachezaji kutoka nje ya Nchi.
Upande wa Wanawake jumla ya wachezaji 16 tayari wamethibitisha na tayari wamesharipoti eneo la tukio.
Makamu Mwenyekiti, Sabri Mohamed wa Chama cha Pool Tanzania, aliitaja mikoa ambayo mpaka sasa inashiriki kuwa ni pamoja na Mbeya, Iringa,Morogoro, Dodoma, Manyara,Pwani, Zanzibar na wenyeji Dar es Salaaam.
Sabri alisema ushindani mwaka huu utakuwa mkubwa sana ukilinganisha na miaka mingine hivyo tunategemea mchezo mzuri na wenye burudani ya kusisimua.
Nae katibu pia alizataja zawadi za washindi kuwa upande wa timu Wanaume, Bingwa atazawadiwa pesa taslimu shilingi laki tano(500,000/=) pamoja na kikombe, mshindi wa pili timu ni shilingi laki moja(100,000/=) na msihindi wa tatu timu ni shilingi elfu hamsini(50,000/=).
Upande wa wachezaji mmoja mmoja(Singles) bingwa atazawadiwa pesa taslimu shilingi laki tano(500,000/=) pamoja na kikome, wa pili shilingi laki moja(100,000/=) na wa tatu shilingi elfu hamsini (50,000/=)
Katibu alisema mashindano hayo yanaushiriki wa jinsia ya kike pia ambapo bingwa atazawadiwa pesa taslimu shilingi laki tatu(300,000/=) na wa pili shilingi laki moja(100,000/=).
Mratibu wa Mashindanio alimaliza kwa kumtaja Bingwa mtetezi wa Mashindano hayo kwa upande wa timu ni Klabu ya Snipers yenye makazi yake Mwenge mpakani jijini Dar es Salaam, upande wa mchezaji mmoja mmoja(Singles) Wanaume, ni Baraka Jackson kutoka Manyara na upande wa Wanawake Singles ni Jackline Tido kutoka Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa, Wilfred Makamba alitoa wito kwa Makampuni na Wadau mbalimbali kutoa sapoti kwenye mchezo wa Pooltable kwani mpaka sasa hakuna mfadhili yeyote aliyejitokeza kusaidiakufanikisha mashindano hayo bali ni juhudi za watu wachache wapenda mchezo.
Msanii wa nyimbo za Mashairi na mchezaji wa timu ya Skylight B, Mrisho Mpoto(Mjomba) akicheza dhidi ya timu ya Vegas ya Sinza wakati wa masindano ya nane nane yanayoendelea katika Hoteli ya Nefaland Manzese jijini Dar es Salaam.Vegas ilishinda 13 – 1.
Mratibu wa Mashindano ya Nanenane, Michael Machela(katikati) akipiga makofi pamoja na Wachezaji mbalimbali wanaoshiriki mashindano hayo mara baada ya uzinduzi uliofanyika katika Hoteli ya Nefaland Manzese jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment