Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ETSIPL (Exhibitions & Trade Services India Pvt. Ltd.) akizungumza na wanahabari kuwaelezea juu ya maonyesho ya pili ya Utabibu na Maabala ya Afrika Mashariki maarufu kama ‘Pharmatech East Africa’ yanayorajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Agosti 24 hadi 26, mwaka huu. Kulia ni Rais wa Chama cha Wafamasia nchini (PST), Fadhili Hezekiah na kushoto ni Mwenyekiti wa TAPI Bw. Churchill Katwaza.
Rais wa Chama cha Wafamasia nchini (PST) akizungumza na wanahabari kuwaelezea juu ya maonyesho ya pili ya Utabibu na Maabala ya Afrika Mashariki maarufu kama ‘Pharmatech East Africa’ yanayorajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Agosti 24 hadi 26, mwaka huu. Kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ETSIPL (Exhibitions & Trade Services India Pvt. Ltd.)
Mwenyekiti wa TAPI Bw. Churchill Katwaza akifafanua jambo mbele ya wanahabari waliohudhuria mkutani uliokuwa ukizindua maonyesho ya pili ya Utabibu na Maabala ya Afrika Mashariki maarufu kama ‘Pharmatech East Africa’ yanayorajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Agosti 24 hadi 26, mwaka huu. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ETSIPL (Exhibitions & Trade Services India Pvt. Ltd.)
Bw. Joseph Mhagama wa Chama cha Watoa Huduma Binafsi za Afya Tanzania (APHFTA) akifafanua jambo.
Bi. Glory Matemu kutoka , Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) akifafanua jambo.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG
Watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuhudhuria katika maonyesho ya pili ya Utabibu na Maabala ya Afrika Mashariki maarufu kama ‘Pharmatech East Africa’ yanayorajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Agosti 24 hadi 26, mwaka huu.
Hayo yameelezwa na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ETSIPL (Exhibitions & Trade Services India Pvt. Ltd.) ambao ndiyo waandaaji wa maonyesho ya Kimataifa ya Kibiashara kutoka India, Digvijay Singh wakati akiongea na wanahabari kuyakaribisha makampuni na hospitali kujitokeza kwa wingi kushiriki.
Singh amesema Tanzania imekuwa ya bahati kubwa, kwani makampuni makubwa yanakuja kuonesha bidhaa zao ambapo itachagiza fursa za uwekezaji.
Maonyesho ya pili ya Kimataifa ya Kitabibu na Maabala yamelenga katika kutoa elimu ya Madawa, APIs, Matibabu, Afya, Upasuaji, Maabala, Mifupa, Usafishaji wa vyumba, Kinywa na masuala mengine yahusuyo sekta ya afya kwa ujuma. Mwaka huu maonyesho haya yamefadhiliwa na BLISS GVS PHARMA LIMITED.
Kwa upande wake Rais wa Chama cha Wafamasia nchini (PST), Fadhili Hezekiah amesema hadi sasa zaidi ya kampuni 105 zimeshathibisha ushiriki wake katika maonyesho hayo.
“Tunashukuru Mungu maandalizi tunaendelea kuyakamilisha maonesho haya ni mahususi na muhimu kama Taifa kuweza kujitokeza kujionea kujifunza kwani ni ya kwanza na ya kipekee kwa Tanzania hasa sekta ya afya.
Amewataka wadau ikiwemo vyuo vya famasi nchini kujitokeza kwa wingi kujionea maonesho hayo kwani ni sehemu ambayo watajifunza na kupata mashirikiano.
‘’Makampuni yataonesha bidhaa zao ikiwemo dawa na vifaa tiba, tutaona dawa kuanzia hatua ya awali hadi inapokuja kuwa dawa… pia amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi maana mwaka huu huduma mbali mbali za kitabibu zitatolewa na vyama vya kitaaluma.
Vile vile ameongeza kuwa kutakuwa na vitu zaidi kutoka kwenye makampuni haya makubwa duniani, ikiwemo Bara la Ulaya, Asia na kwingine,” amesisitiza.
‘’Kampuni kubwa kutoka nchi kama India, Uganda, Misri, Kenya, Rwanda na nyingine nyingi Bara la Ulaya, zinakuja kuonyesha bidhaa zao, dawa na vifaa tiba… ambapo pia itakuwa ni fursa za wao kuwekeza hapa nchini, hivyo wadau na watu mbalimbali waje waone ni bure kabisa,’’
amesema Hezekiah.
Aidha, maonyesho hayo pia yanawezeshwa na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali kupitia Wizara ya Afya, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Chama cha Watoa Huduma Binafsi za Afya Tanzania (APHFTA), Chama cha Waingizaji wa Dawa za Binadamu (TAPI), Chama cha Wazalishaji wa ndani wa Dawa za binadamu (TPMA), Chama cha Madaktari Bingwa wa Upasuaji Tanzania (TSA), Chama cha Madktari Wanawake (MEWATA) na Chama cha Wazalishaji wa dawa na vifaa tiba Tanzania (TMDMA). Maonyesho haya yanasimaniwa na TANTRADE pamoja na wadau wa ndani ikiwem wadau wa Tanzania Conference Services Ltd na Crayon Media Agency respectively.
No comments:
Post a Comment