HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 29, 2023

MAOKOTO DEILEE YASHIKA KASI

 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

PROMOSHENI ya Maokoto Deilee inayoratibiwa na Kampuni ya Michezo ya Kubashiri (Sportpesa) kushirikiana na Mtandao wa simu za mkononi, Tigo imeendelea kushika kasi kwa wateja mbalimbali kujishindia fedha na simu janja.

Akizungumza kwenye droo ya kwanza iliyofanyika Karume, Ilala jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Sportpesa, Sabrina Msuya amesema kupitia droo hiyo ya kwanza tayari simu ya mkononi (simu janja) imenyakuliwa na mshindi sanjari na kiasi cha fedha shilingi Milioni moja (Tsh. 1,000,000/-).

“Mshindi mmoja kutoka Kigoma tayari amejishindia simu janja na mshindi mwingine kutoka Mtwara, wilayani Newala amejishindia fedha taslimu, kiasi cha shilingi Milioni moja katika droo ya wiki hii,” amesema Msuya.

Msuya amesema kila wiki, watafanya droo hiyo kwenye maeneo ya wazi na kutangaza washindi hadharani ili kutoa nafasi kwa wateja kushuhudia droo hizo. “Hata droo ya mwisho ambayo mshindi atashinda kiasi cha fedha shilingi Milioni 15 (Tsh. 15,000,000) tutafanya hadharani,” ameeleza Msuya.

Mwakilishi wa Mtandao wa Tigo, Afisa wa Tigopesa, Kelvin Felician amewahimiza wateja mbalimbali kuendelea kubashiri michezo mbalimbali kupitia tigopesa huku akisisiza kuwa wataendelea kutoa zawadi za fedha na simu janja kushirikiana na Sportpesa.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Sportpesa, Sabrina Msuya akizungumza na waandishi wa habari sanjari na wateja mbalimbali wa mchezo wa kubashiri wakati wakitoa zawadi ya droo ya kwanza ya Maokoto Deilee ambayo inaratibiwa na Sportpesa kushirikiana na Mtandao wa Simu, Tigo. Droo hiyo imefanyika eneo la Karume, Ilala - Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad