HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 1, 2023

Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango aipongeza NIC Insursnce kwa kutoa bima za kilimo

 Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango akipata Maelezo kuhusiana na NIC kuwa kampuni ya kwanza kutoa bima za kilimo kutoka kwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati alipotembelea banda la NIC Insurance kwenye Ufunguzi wa aonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Mbeya

MAKAMU wa Rais Dkt.Philip Mpango ameipongeza NIC Insurance kwa kuwaponya wakulima kwa changamoto zinapowakuta wa kilimo.

Dkt.Mpango ameyasema hayo wakati alipotembelea banda la NIC kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nyanda za Juu Kusini yanayofanyika katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Dkt.Mpango amesema kuwa NIC Insurance iendelee kutoa elimu zaidi kuhusiana bima za kilimo kwa kuongeza wigo wakulima kufikiwa na bima.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema NIC Insurance ni kampuni ya kwanza kutoa bima ya kilimo ambayo imesaidia wakulima.

Bashe amesema kuwa mwaka juzi NIC Insurance ililipa bima kwa baadhi ya mazao mbalimbali waliokumbwa na majanga.

Hata hivyo amesema kuwa amesema kuwa kazi iliopo ni kuongeza uwigo mazao mbalimbali katika kuhakikisha wakulima wanakuwa na uhakika pale wanapopata majanga.
Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango akisoma kipeperushi cha taarifa cha NIC Insurance wakati alipotembelea banda la NIC Insurance kwenye Ufunguzi wa Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango akipokelewa na Meneja wa NIC Insurance Justine Iseni wakati alipotembelea banda la NIC Insurance kwenye Ufunguzi wa Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad