HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 9, 2023

KAJALA ALAMBA UBALOZI LUNA AFUNGUKA MAZITO YA ANJELLA KUSEPA KONDEGANG

 



Na Khadija Seif, Michuziblog
MSANII Wa Bongomuvi Kajala Masanja afunguka na kushangazwa na tuhuma zinazomkabili kuhusishwa na chanzo ni yeye kuondoka kwa Msanii Angella katika Lebo ya Kondegang .

Akizungumza na Wanahabari Leo Agosti 09,2023 Kajala Masanja mara baada ya kupewa Ubalozi wa taulo za kike aina ya "Luna" Jijini Dar es salaam ,amesema anajivunia kuona kampuni mbalimbali zinaendelea kumuamini na kuona anaweza kutangaza bidhaa zao kupitia tasnia yake licha ya kupitia changamoto mbalimbali za kuchafuliwa mitandaokwa skendo.

Hata hivyo Kajala ameeleza kwa namna amekuwa akitumia bidhaa hiyo ya Luna na kuhaidi kuwa balozi mzuri wa kuhakikisha inawafikia watu wote hususani wasichana wadogo Mashuleni.

Pia Kajala ameongeza kuwa hausiki na kuondoka kwa Msanii Angella kutoka Lebo ya Kondegang kama inavyosambaa mitandaoni ikimuonesha Anjella kulalamika kuwa chanjo cha kuondoka kwake ni Kajala ambae alikuwa Mchumba wa Mkurugenzi wa Lebo hiyo (Harmonize)

"Nimekuwa nikijitahidi kuwasilisha taarifa kuhusiana na Msanii wakike wa Lebo ya Kondegang Anjella kutaka kuondoka lebo hiyo na kumuomba Mkurugenzi wa Lebo Harmonize kumpatia Ajella gari ili aweze kujikimu kutokana na ulemavu alionao lakini huwezi zuia mtu kusema au pia huwezi jua na watu wanamzunguka huwa wamempa sumu gani ili nionekana sina msaada kwake."

Nae Afisa Masoko wa Kampuni ya Luna Jackline Lesika ameeleza sababu ya kumchagua Kajala kuwa balozi wa Luna ni kutokana na umaarufu wake ,Kuwa Mama na mtu ambae anajua bidhaa bora na salama kwa wanawake hususani kuhakikisha Afya ya uzazi inakua imara.

"Tunajua wazi kuwa kwa Mwanamke anaefikia miaka 40 na zaidi huwa anakoma hedhi swali linakuja kwa Balozi huyu sababu hasa ya kupewa ubalozi ni kutokana na yeye ni mama wa binti (Paula) hivyo anajua kipi sahihi cha kumfaa binti yake huyo na mabinti wengine wengi kutokana na kujua changamoto zote za hedhi ."
Picha ya pamoja Kati ya Meneja Masoko wa Kampuni ya Taulo za kike aina ya Luna Jackline Lesika katikati Balozi mpya wa Taulo hizo Kajala Masanja, kushoto kwake Mkurugenzi wa Kampuni ya Taulo za Luna Steven Swai wakiwa kwenye Mkutano na Wanahabari Leo Agosti 09,2023 Jijini Dar es salaam mara baada ya kutangazwa kwa Msanii Kajala Masanja kama Balozi mpya wa taulo za Luna

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad