HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 10, 2023

JKT, WIZARA YA KILIMO WASAINI MKATABA WA MASHIRIKIANO KUINUA SEKTA YA KILIMO

 

Wizara ya Kilimo na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakibadilishana hati za makubaliano kwa ajili ya Vijana wa Program ya BBT kupata mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kushudiwa na Rais na Amir Mkuu Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Wizara ya Kilimo na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakionesha hati za makubaliano kwa ajili ya Vijana wa Program ya BBT kupata mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kushudiwa na Rais na Amir Mkuu Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Wizara ya Kilimo na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakisiani makubaliano kwa ajili ya Vijana wa Program ya BBT kupata mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa


Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limeingia makubaliano na Wizara ya Kilimo kutekeleza agizo la Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa Program ya Vijana ya Kujenga Keshi iliyobora (BBT).

Akizungumza mara baada ya kuhitimishwa Maonesho Kitaifa ya Kilimo Nane Nane yalifanyika jijini Mbeya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema kuwa makubaliano waliongia na Wizara mbili ni kuwachukua vijana walioko katika mradi wa BBT kupata mafunzo ya kuwajenga katika uzalendo na ukakamavu wakiwa katika mashamba kuwa na uvumilivu.

Amesema kuwa vijana wataopata mafunzo watanufaika katika sekta za kilimo pamoja na mifugo kuwa mfano wa kuigwa na vijana wengine kuingia katika sekta hizo.

Meja Jenarali Mabele amesema wametiliana saini mkataba wa mashirikiano katika kutekeleza mradi wa mashamba makubwa kuwezesha vijana kulima, kibiashara kwenye mradi huo Building a Better Tommoow (BBT)

Amesema makubaliano hayo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Naye Mkuu wa Huduma za Sheria wa Jeshi Kujenga Taifa (JKT) Kanali Projestine Rutaiwa amesema mafunzo ya vijana wa BBT yataratibiwa kwa ushirikiano wa wizara hizo.

Amesema kuwa makabaliano hayo kwa mafunzo watayoyapata yataleta matokeo chanya katika vijana hao kwenda kutekeleza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad