Kampuni ya Gf Trucks &
Equipment’s Ltd ya jijini Dar es Salam imeibuka mshindi wa Pili wa Banda
Bora kwa makampuni yanayotoa huduma ya uuzaji wa mitambo na magari
Migodini .
Hayo yamebainika wakati wa kuhitimisha Maonyesho ya
Madini na Uwekezaji yaliofanyika Rwangwa mkoani Lindi yalioanza tarehe
21 na kuhitimishwa na Waziri mkuu Kasimu Majaliwa aliye ambatanana na
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ambae alikua mgeni Rasmi
Akizungumza wakati wa ufungaji wa Maonyesho hayo Kikwete alisema Wakati
anastaafu aliiacha Rwangwa ikiwa haiku hivi na amekuja ameikuta Rwangwa
ile nah ii ya sasa ni Mbingu na Aridh kutokana na uwe,kezaji wa madini
na fursa zilizopo mkoa wa Lindi kwenye Madini hivo mabadiliko ni makubwa
mmno.
Nae Afisa Mauzo wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s
Ltd , Peter William alisema wao kama Gf wamejikita kuhakikisha
wanawakomboa wachimbaji wa dogo na wakati kwa kuanzisha mapango maalumu
wa kuhaikisha wanawawezesha wachimbajinchini kupata mitambo ya kuchimbia
kwa gharama nafuu kwa kushirikiana na tasisi za Kibenki wameazisha
utaratibu wa kumkopesha mashine (matambo )iki kuweza kufanya kazi kwa
uharaka Zaidi.
Pia Peter alisema wamejipanga kuwekeza nguvu
Zaidi na hivi karibuni watafungua ofisi katika ukanda wa kusini ili
wateja wasipate usumbufu wa kuja hadi Dar es salaam.Kampuni ya Gf
inayojishungulisha na uuzaji wa Magari ya FAW, FORLAND,HONG YANG
(trucks) pamoja na mitambo ya XCMG maalumu kwa shuguli za migodini na
Wakandarasi wa Barabara.
Akihitimisha maonyesho hayo Waziri mkuu
Kassim Majaliwa ametoa onyo kwa maafisa wanaohusika na utoaji wa leseni
za madini kuacha tabia ya kuwazunguka wananchi wanaokwenda katika ofisi
zao kuomba leseni za uchimbaji baada ya kubaini uwepo wa madini kwenye
baadhi ya maeneo na kisha kuwapa wachimbaji wengine.
”…Acheni
tabia ya kuwaonea wananchi wanaotoka kwenye maeneo yenye fursa ya madini
anakuja kuomba leseni ya kumiliki eneo hilo na unamwambia aache taarifa
zake aje kesho kuchukua majibu akija kesho unamwambia eneo hilo
limeshachukuliwa na mtu mwingine kumbe wewe unamtafuta mtu wa kuweza
kumiliki ili upate chochote kitu, tukikugundua hatua kali zitachukuliwa
dhidi yako. ”
Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Agosti 26, 2023) wakati
akifunga Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji mkoani Lindi
yaliyofanyika kwenye viwanja vya soko la Kilimahewa wilayani Ruangwa.
Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha uwepo wa mazingira bora
kwa wawekezaji wa ndani na nje.
Pia, Mheshimiwa Majaliwa
ameuagiza uongozi wa Wakala wa Jiolojia Tanzania ufanye tafiti za madini
za kimkakati kwa kushirikiana na halmashauri kwa lengo la kuwasaidia
Watanzania kufanya shughuli zao kwa tija na kuhakikisha mipango sahihi
ya matumizi ya ardhi inafikiwa.
Afisa Mauzo wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd , Peter William akiwa ameshikilia Zawadi ya Tuzo kwa kuwa kampuni ya pili kwa utoaji wa uuzaji wa magari na mitambo migodini wakati wa maonyesho ya madini Rwangwa
Banda bora
Tuzo
No comments:
Post a Comment