Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mobhare Matinyi akizungumza na wafanyabiashara wa matunza katika ziara aliyoifanya kwenye soko la Tazara.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mobhare Matinyi akiskiliza jambo kutoka kwa mwakilishi wa wauza Matunda katika soko la Tazara Jijini Dar es Salaam.
Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
MKUU wa Wilaya ya Temeke Mheshimiwa Mobhare Matinyi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya, leo Agosti 11, 2023 ameambatana na Kamati ya Siasa ya Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kufanya ziara soko la Tazara ikiwa ni katika kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Akiwa katika soko hilo Mhe . Matinyi ametoa wito kwa wafanyabiashara sokoni hapo kufanya usafi ili kujiepusha na magonjwa ya milipuko na kuzingatia afya za watumiaji wa soko hilo maarufu kwa kuuza matunda.
"Pamoja na mikikimikiki ya masoko ilivyo, lakini tusikubali kuishi katika hali ya uchafu, Kamati za mazingira kwenye Kata na Mitaa yetu tushirikiane kuhakikisha maeneo yetu yanakuwa safi" amesema DC Matinyi.
Aidha Mhe. Matinyi amekagua mradi wa uboreshaji miundombinu katika maeneo ya wafanyabiashara ndogondogo sokoni hapo na kusikiliza changamoto za wafanyabiashara hao ikiwemo ulipaji wa ushuru wa Manispaa.
Kaimu Mkurugenzi Wakili Faraja Nakua ameuomba uongozi wa soko hilo la Tazara kuratibu mapendekezo ya kipi kifanyike kwenye upande wa ushuru na kuahidi kuwa Halmashauri ipo tayari kukaa na kupitia kwa maslahi ya pande zote.
Usafi kwenye maeneo ya makazi na biashara ni mojawapo ya mambo ambayo DC Matinyi amekuwa akishughulikia tangu alipoteuliwa na Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan.
No comments:
Post a Comment