HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 21, 2023

YANGA NA GSM YATEMBELEA VITUO VYA KULEA WATOTO WIKI YA MWANANCHI

 

 Kuelekea siku ya mwananchi ambayo itafanyika Jumamosi, tarehe 22 Julai 2023, Makampuni ya GSM Group kwa kushirikiana na klabu ya soka ya Young Africans (Yanga), wameshiriki katika “wiki ya mwananchi” ambayo ni maalumu kwa ajili ya mashabiki wa Yanga kote nchini.

Kama mdhamini rasmi wa klabu ya Yanga, GSM Group imeshiriki wiki ya mwananchi siku ya Ijumaa ya tarehe 21 Julai, 2023 kwa kutoa msaada katika vituo vya kulea watoto vilivyopo Buguruni na Vingunguti na kuwapatia mahitaji muhimu kama vile chakula, sabuni na vifaa vya usafi, runinga (TV) kutoka Haier pamoja na mahitaji mengine.

GSM Group na Haier wanajivunia kushiriki katika wiki ya mwananchi ikiwa sehemu ya shukrani kwa sapoti ambayo makampuni hayo yanaipata kutokana na udhamini wa Yanga. GSM Group inaamini moja ya jukumu la kuwa sehemu ya jamii ni kusaidia na kutunza makundi yaliyopo katika hatari na kuhakikisha mahitaji yao yanatimizwa hata kama sio mashabiki wa mpira wa miguu. GSM Group pia inatoa ari kwa mashabiki wa mpira na jamii nzima kwa ujumla kushiriki katika matukio kama haya ambayo yatasaidia kuitunza jamii yetu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad