Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
KAMPUNI
ya Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Limited imegawa mitungi na majiko yake
500 kwa Wenyeviti na Watendaji wa Vijiji na Kata zote za Halmashauri ya
Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga huku ikieleza lengo la kugawa mitungi
hiyo ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia katika kuhamasisha matumizi ya
nishati safi ya kupikia nchini.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa
mitungi hiyo mbele ya viongozi hao wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya
Korogwe Jokate Mwegelo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Araman
Benoite amesema wamekuwa wakiendelea kufanya uwekezaji mkubwa nchini
Tanzania kwa makundi mbalimbali ya wananchi ili kuunga mkono juhudi za
serikali.
"Serikali imeendelea kuhamasisha matumizi ya gesi safi
ya LPG ambayo ni suluhisho la kuondoa matumizi ya kuni na mkaa, hivyo
basi kuboresha afya ya jamii na kulinda mazingira,sambamba na ahadi ya
Rais kutoa nafasi ya matumizi ya nishati safi ya kupikia."
Aidha
amesema katika muendelezo uleule wa juhudi za kuhamasisha matumizi ya
nshati safi ya kupikia kwa wananchi wote,kampuni ya Oryx Gas imeamua
kusimama na wananchi wa wilaya ya Korogwe mkoani Tanga kupitia kwa
viongozi wao kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wote.
"Juhudi
hizi ni pamoja na kusaidia kuwabadilisha viongozi wa wananchi kuachana
na kuni na mkaa na kuhamia kwenye nishati ya gesi za kupikia (LPG).Hivyo
tumekabidhi mitunge ya gesi na majiko 500, " amesema na kuongeza
ugawaji huo umekwenda sambamba na kutoa mafunzo ya usalama wa matumizi
ya mitungi hiyo.
Benoite amesema wanaamini viongozi wanawakilisha
wananchi na kiongozi anapaswa kuongoza kwa mifano na wanaushawishi
mkubwa kwa wananchi wanaowaongoza hivyo Oryx imeona itoe mitungi ili wao
wenyewe wakianza kutumia watape mamlaka ya kuwaambia wananchi umuhimu
wa mabadiliko.
Pia amesema Oryx Gas Tanzania Ltd inaendelea
kuwekeza katika uagizaji, uhifadhi, ujazaji wa gesi kwenye mitungi na
usambazaji wa LPG Tanzania nzima, pamoja na Visiwa vyake. Oryx Gas
Tanzania huwekeza kila mwaka mamilioni kadhaa ya dola kwenye mitungi
mipya inayoingizwa sokoni kila siku.
Kwa upande wake Mkuu wa
Wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo amesema ugawaji wa mitungi hiyo ya gesi
inakwenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha matumizi ya
nishati safi ya kupikia kwa wananchi ikiwa ni kuunga mkono juhudi za
Serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ambaye alishazindua
kampeni ya kutumia nishati mbadala kwa lengo la kulinda mazingira.
Amesema
katika wilaya hiyo wameamua kugawa mitungi hiyo ya gesi kwa viongozi
mbalimbali kuanzia ngazi ya wilaya mpaka ngazi ya msingi wakiwemo
wenyeviti wa vijiji na watendaji katika kata zote huku akifafanua lengo
kubwa ni kutoa ujumbe kwamba miti mingi inayokatwa iko vijijini na huko
ndiko ambako viongozi hao wapo.
”Wenyeviti na watendaji wa vijiji
tumewaona na tumetambua uwepo wenu, kama viongozi kwenye maeneo yeenu
kuna watu wanawaakangalia. Leo hii mwenyekiti wa kijiji na mtendaji wake
wakiamua kutumia nishati mbadala na wanakijiji watahamasika.
"Kwasababu
wanaangalia viongozi wao wanawajua, wamewachagua wenyewe na wana uwezo
wa kuwashawishi kuacha kutumia miti vibaya wakaanza sasa kuunga mkono
jitihada hizi za kutumia nishati mbadala ili tuokoe kizazi hiki na
kinachokuja."
Aidha
ameeleza kutokana na uharibifu wa mazingira Serkali ilitoa maelekezo
mahususi wananchi kupandeni miti na kutunza mazingira , vyanzo vya maji
ili kupata maji lakini kilimo kibaki salama kuwe na chakula cha kutosha.
“Sasa
maamuzi ni ya kwetu sisi, na ndio kwenye haya nikasema lazima sisi
viongozi katika ngazi zote ndani ya wilaya ya Korogwe tukubaliane
tuachane na matumizi ya mkaa na kuni.Tukiamua kubadilika tutachochea
wenzetu kubadilika.
“Nikasema sipendi kushurutisha watu bila
kuwezesha , majiko ya gesi ndio haya kazi kwenu , lakini hii ni awamu ya
awali tumeshauriana na viongozi wenzangu hivyo tutaenda awamu kwa
awamu.Nia yangu ni kuwa na Korogwe inayosomeka kama wilaya kinara kwenye
matumizi ya nishati safi,”amesema Jocate.
Ameongeza suala la
nishati safi ya kupikia ni la wote hivyo watalibeba kwa mikono miwili
ili kunusu misitu na mazingira sambamba na kwenda na kauli ya Rais
Dk.Samia ya kuigeuza Tanzania salama na yenye kusifika katika utunzaji
mazingira na kutumia nishati safi ya kupikia.
“Huo ndio mtazamo
wetu na katika kufanikisha tumeungwa mkono na wenzetu wa Oryx ambao
wanasifika kwa kugawa mitungi lakini mimi ningependa wasifike kwa watu
unaowagawia mitungi waendelee kutumia hii mitungi.Watu lazima waendelee
kutumia gesi na hii iwe endelevu,"amefafanua.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo(katikati) ,Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Tanzania Araman Benoite (wa pili kulia) pamoja na Meneja Mauzo Ukanda wa Dar es Salaam na Pwani Shaban Mohamed(wa tatu kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi Rose Kimweri ambaye ni miongoni mwa viongozi na mjasiriamali katika wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Jokate Mwegelo (katikati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Araman Bonoite (wa pili kulia) wakimkabishi mtungi wa gesi ya Oryx pamoja na jiko lake Mjumbe wa kikundi cha Lutind Tea Herbs and Spices Mariam Angeline Isidor .Wengine katika picha hiyo ni viongozi wa ngazi mbalimbali katika wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.Meneja Masoko wa Oryx Gas Tanzania ( kushoto) akitoa maelezo kuhusu usalama wa utungi wa gesi la Oryx kwa watendaji na wenyeviti wa kutoka kata zote za Wilaya ya Korogwe, Wa kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Tanzania Araman Bonoite
Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx GasTanzania Araman Benoite akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wenyeviti na watendaji wa Wilaya ya Korogwe kuhusu namna salama ya kuutumia mtungi wa gesi.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo akiwa amekata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa duka la kuuza mitungi ya Oryx Gas wilayani Korogwe
No comments:
Post a Comment