HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 19, 2023

WAZIRI NDALICHAKO AITAKA BODI YA ATE KUENDELEZA MAHUSIANO MAZURI NA MAJADILIANO YA UTATU

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

BODI ya Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) imetakiwa kuendelea kutoa nafasi kwa vijana kupata ajira pamoja na nafasi za mafunzo kwa vitendo sehemu za kazi ili kuweza kuwajengea ujuzi kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.

Akizungumza leo Julai 19,2023 Jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa 63 wa Bodi ya ATE, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Ndalichako amesema anaimani Bodi itaendelea kuwa chachu ya kukipeleka Chama mbali zaidi na kuboresha yale ambayo wanafanya na hata kuleta mengine mazuri zaidi huku wakiendeleza mahusiano mazuri na majadiliano ya UTATU.

Aidha ameihakikishia Bodi kutoa ushirikiano katika kukuza na kuendeleza sekta ya kazi na ajira nchini.

Ninatambua kuwa Sekta ya Ajira na Kazi ina changamoto mbalimbali ambazo sisi kama Serikali tunaamini ufumbuzi upo katika kushirikiana nanyi. Matatizo haya ni kama vile ukosefu wa ajira, ukosefu wa ujuzi kwa vijana na nafasi za kujifunza kazi ambazo Serikali imeendelea kutumia mbinu mbalimbali kuzipunguza na kuzitatua

Amesema kupitia Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano, awamu ya tatu wamelenga kupunguza ukosefu wa ajira kutoka asilimia 9 (mwaka 2019) kufikia asilimia 8 ifikapo mwaka 2025/26.

Ameeleza kuwa kukuza ujuzi ni kati ya mipango iliyobainishwa na Serikali ili tufikie lengo na kuongeza idadi ya wahitimu waliopata mafunzo mahala pa kazi ni njia mojawapo ya kukuza ujuzi nchini kwa vijana.

“ama nchi tunatazamia kuongeza idadi ya wahitimu wenye mafunzo ya uanagenzi kufikia 231,000 ifikapo mwaka 2025/26 kutoka 46,000, mwaka 2019/20. Vivyo hivyo, kwa mafunzo tarajari, lengo ni kufikia wahitimu 150,000 ifikapo mwaka 2025/26 kutoka 30,000, mwaka 2019/20”. Amesema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bw. Oscar Mgaya ameahidi wataendeleza mahusiano na wadau wa UTATU ili kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini kwa ustawi wa Sekta ya Kazi na Ajira kwa kufuata misingi ya Katiba ya Chama lakini pia Sheria, Kanuni na Taratibu

"Kupitia vikao vyetu vya UTATU tutaendelea kutoa mchango wetu katika kufikia malengo haya. Pia ni muhimu kuwa Business agenda hii imenyambuliwa kutoka kwenye Blue print". Amesema

Pamoja na hayo ameipongeza Serikali kupitia Sheria ya Fedha ya Mwaka 2023 imepunguza Tozo ya Kuendeleza Ujuzi (SDL) kutoka asilimia 4 hadi asilimia 3.5 na kuahidi kuipunguza taratibu ili kuendela kuwapunguzia waajiri gharama za kufanya baishara nchini.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza katika Mkutano wa 63 wa Bodi ya Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) uliofanyika leo Julai 19,2023 Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bw. Oscar Mgaya akizungumza katika Mkutano wa 63 wa Bodi ya Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) uliofanyika leo Julai 19,2023 Jijini Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa ATE, Bi. Suzanne Ndomba-Doran akifanya wasilisho kuhusu Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na namna kinavyofanya kazi huku akigusia muundo wake, majukumu yake na namna kinavyoshirikiana na wadau wake katika Mkutano wa 63 wa Bodi ya Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) uliofanyika leo Julai 19,2023 Jijini Dar es Salaam.


Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama Cha Waajiri Tanzania, (ATE) wakiwa kwenye
Mkutano wa 63 wa Bodi ya Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) uliofanyika leo Julai 19,2023 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad