HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 10, 2023

Rais Samia Suluhu Hassan ahudhuria Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya JKT, Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma tarehe 10 Julai, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajab Mabele wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma tarehe 10 Julai, 2023.

Gwaride la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) likipita kwa mwendo wa pole na haraka mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma tarehe 10 Julai, 2023.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati wa Wimbo wa Taifa ukiimbwa katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma wakati wa kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) tarehe 10 Julai, 2023.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad