HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 7, 2023

SERIKALI IHARAKISHE KULETA HUDUMA YA MAWASILIANO -MLATA

 

 

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Mkoa wa Singida Martha Mlata ameiomba Serikali kuharakisha kupeleka huduma ya mawasiliano ya mtandao katika Kata ya Makilawa.

Mlata amayasema hayo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wq Ilani pamoja na kusikiliza kero za wananchi ambapo ametumia nafasi hiyo kutoa ombi kwa serikali kuangalia uwezekano wa kuharakisha kupeleka huduma hiyo ya mtandao wa mawasiliano ya simu kwa wananchi wa kata hiyo

Aidha Mlata ambaye ameambatana na Kamati ya Siasa ya Mkoa , ametumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuebdelea kutekeleza miradi mbalimbali kwa lengo la kuleta maendeleo.

"Naipongeza kwa kazi nzuri ya kusimamia miradi ya maendeleo lakini tunaona iko haja kwa Serikali kuharakisha kuleta huduma mawasiliano ya mtandao ya simu ili wananchi wawe na urahisi katika kufanya mawasiliano."


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad