HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 13, 2023

Maisha Magic Bongo yaja na vipindi vipya Wimbi & Diva &Hustlers!


· Wimbi kuleta vionjo vipya kwa wapenzi wa tamthilia Tanzania

· Malkia Karen, Kinata MC, Chinno Kid rasmi ndani ya DStv na vibe kama lote!

Mambo yanazidi kupamba moto ndani ya chaneli maarufu ya Maisha Magic Bongo ndani ya DStv ambapo imezindua vipindi vyake vipya vya Wimbi sambamba na Divas & Hustlers kwenye chaneli ya Maisha Magic Bongo mwezi huu wa Julai. Vipindi hivi vya kuvutia vitapatikana kwenye chaneli ya Maisha Magic Bongo, DStv CH. (160). Uzinduzi huu unathibitisha jitihada za DStv katika kuwapa wateja wetu chaguo bora la vipindi na huduma ya televisheni kwa gharama nafuu.

Akizungumza katika hafla ya kuzindua vipindi hivyo vipya vya chaneli ya Maisha Magic Bongo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania Bi. Jacqueline Woiso amesema kuwa "Tunafurahi kuwatambulisha watazamaji wetu vipindi vipya vya kusisimua vya 'Wimbi' na 'Divas and Hustlers. Kuingizwa kwa vipindi hivi vipya ndani ya DStv kumezingatia sana maoni ya watazamaji na tunaamini kuwa watavifurahia sana.

Wimbi" ni tamthilia ya Kitanzania inayolenga visa vya mapenzi, tamaa, mali, na siri za familia. Tamthilia hii itakuwa inarushwa kila Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia saa 4:00 usiku, kwenye chaneli ya Maisha Magic Bongo, DStv Ch. (160).

Tamthilia hii pia itakuwa na wasanii maarufu na wakongwe akiwemo Blandina Chagula maarufu kama Johari, Natasha Ma Mvi, na Yusuph Mlela na wengine wengi. "Wimbi" ilianza kuonekana hewani tarehe 3 Julai 2023, na tunaiimani itawavutia wapenzi wa tamthilia kwa hadithi yake ya kusisimua na uigizaji bora.

Aidha, "Divas and Hustlers" itaanza kurushwa siku ya Alhamisi, tarehe 13 Julai 2023, na itapatikana pia katika chaneli ya Maisha Magic Bongo, DStv Ch. (160), kila Alhamisi saa 3:00 usiku.

Kipindi hiki kinashirikisha mastaa maarufu kama vile Chinno kid mcheza mziki maarufu, mwanamuziki Malkia Karen, mkali wa singeli Kinata MC, Rey Jones, na wengine wengi. "Divas and Hustlers" imejipanga kuleta Mapinduzi ya burudani kupitia watu hawa mashuhuri katika tasnia ya burudani hapa nchini.

Kama haitoshi, wateja wa DStv wataendelea kufurahia vipindi vingine kama vile "Jua Kali," inayoruka kila siku ya Jumatano hadi Jumapili saa 3:30 usiku, tamthilia ya "HUBA" Jumatatu hadi Ijumaa saa 3:00 usiku,tamthilia ya "Pazia" Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 usiku, na vichekesho vya "Kitimtim" Jumatatu na Jumanne saa 3:00 usiku.

Aidha, wapenzi wa vichekesho wataendelea kuongeza siku za kuishi kupitia vichekesho vya "Return of Original Comedy" kila Jumapili saa 3:00 usiku na "Watubaki " kila Jumamosi saa 3:00 usiku ndani ya Maisha Magic Poa, DStv Ch. (144), inayopatikana kwenye kifurushi cha DStv Poa kinachopatikana kwa Tshs. 10,000/-

Wapenzi wa soka nao hatujawaacha nyuma, kupitia chaneli zetu za SuperSport, pia tumejipanga kuleta burudani ya moja kwa moja katika msimu mpya wa soka utakaoanza rasmi Agosti 11 mwaka hu, kwa mfumo wa picha anagvu yaani HD, kwa wateja wetu wakubwa wa DStv. Mashabiki wa soka nchini Tanzania wanapaswa kukaa mkao wa kula, DStv kupitia SuperSport itaonyesha mechi zote 380 za Ligi Kuu kwenye chaneli yetu maalum ya SuperSport Premier League Ch. (223) na kuwapa uhuru wa kuchagua kutazama mechi hizo kwa lugha adhimu ya Kiswahili.

Hii haiishi hapa, kupitia SuperSport pia tumejiandaa kuonyesha zaidi ya mechi 300 za kusisimua kutoka La Liga kwenye chaneli yetu ya SuperSport La Liga Ch. (224), pamoja na mechi zaidi ya 300 za kusisimua kutoka katika ligi ya Serie A.

Amewataka wale wote ambao hawajajiunga na DStv kufanya hima kuwahi ofa maalum iliyopo sokoni kwa sasa ambapo mteja hupata seti kamili ya DStv kwa shiling 99,000 tu! Amesema hii ni ofa ya muda maalum hivyo ni vyema wakaichangamkia ili wasipitwe na moto wa burudani unaoendelea kuwaka ndania ya DStv.

Kulipia kifurushi cha DStv bonyeza *150*53# au piga 0659 070707 kujiunga na DStv!
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad