HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 19, 2023

Jinsi Watanzania wanavyoweza kuvuna mamilioni na bikoboost

 

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

ULINGO wa fursa za kiuchumi kupitia mchezo wa kubahatisha wa Biko Tanzania, umezidi kuboreshwa baada ya kampuni hiyo kuzindua promosheni yao inayojulikana kama Bikoboost. Kuzinduliwa kwa promosheni hiyo kwa wateja wa Biko ni maalum kwao ili waingie kwenye kinyang’anyiro cha bahati kwa lengo la kuchota mamilioni ya fedha yanayomwagika.

Biko bahati nasibu ya Watanzania, imekuwa kielelezo madhubuti ya malengo ya kunufaisha wadau wanaotumia eneo hilo kwa ajili ya kujipatia maendeleo tarajiwa.

Tangu ilipoanzishwa nchini, Watanzania wengi kutoka sehemu mbalimbali za nchi wamekuwa wakijishindia zawadi taslimu za fedha, bila kusahau waliowahi kunyakua pia bodaboda na nyumba walizotumia katika maisha yao.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa Biko Tanzania, Charles Mgeta, anasema ni matarajio yao makubwa kuwa mchezo wao utazidi kuwa chanzo kikubwa cha mapato cha Watanzania kulinganisha na michezo mingine.

Anasema wameweka utaratibu mzuri kuruhusu Watanzania washinde fedha kwa urahisi jambo linaloonyesha mafanikio ya dhamira yao kwa nchi.

“Biko ni maisha ya Watanzania wengi wanaoamua kuitumia kwa lengo la kupata fedha zinazokwenda kuboresha maisha yao kila siku, ndio maana mchezo huu umezidi kupendwa na kuungwa mkono.
“Kwa kulijua hilo, ndio maana sasa tumeamua kuboresha zaidi kwa kuingiza sokoni bidhaa mpya inayojukana kama bikoboost, ambapo wateja wanajipangia wenyewe ushindi, ambapo kila mtu anaweza kushinda hadi mara 10 ya ushindi wake,”Alisema.

Mgeta anasema kujipangia ushindi kunatokana na mtu kucheza biko ambapo atakapoweka Sh 5000, pindi atakapotua kwenye ushindi wa Bikoboost, anaweza kuzidisha ushindi wake hadi mara 10.

Akipata Sh 5000 na kucheza mara 10, atakuwa amejipatia zawadi ya Sh 50,000 papo kwa hapo kwenye simu yake. Hatua hiyo inaendelea kwa kiasi chochote ambacho mtu atacheza ambapo ushindi unaanzia Sh 2500 hadi Milioni 10, huku kianzio cha kucheza 0kikiwa ni Sh 1000 na kuendelea.

“Hii ni fursa kubwa kwa Watanzania, ambapo mtu akipokea meseji ya Bikoboost ya ushindi wa Sh 100,000 akaambiwa ajipangie ushindi na akaamua kuweka Sh 10,000 nyingine atashinda Sh Milioni 1,000,000.

“Hii inamaanisha sasa gurudumu la bahati la biko limezidi kuwa tamu, ndio maana zawadi za papo kwa hapo zinamwagika kama njugu na droo kubwa za kila mwisho wa wiki zinaongeza shauku na joto la kuwa mamilionea wa Biko,”Alisema.

Afisa mtendaji huyo anasema ukiwa na buku kwenye simu yako, tayari una biko inayoweza kukupa ushindi wa mara 10 zaidi endapo utaamua kujipangia ushindi kwa kuamua kucheza iwe kwa simu ndogo au wanaotumia simu janja kwa maana ya kutumia mtandao wa www.biko.co.tz.

Mgeta anasema wanaotumia simu ndogo wawatalazimika kuingia kwenye miamala ya simu zao na kuandika namba ya kampuni ambayo ni 505050, huku wakiweka kumbukumbu 2456 au sawa na neno biko na kumalizia namba zao za siri ili waruhusu muamala wa fedha waliyoamua kucheza kwa maana ya sh 1,000 au zaidi.

Katika hatua nyingine, Mgeta anasema wanaotumia simu janja wataingia mtandaoni www.biko.co.tz na kujisajiri kwa njia rahisi ili kuanzisha akaunti zao zinazotokana na namba zao za simu, huku pia wakiweka namba zao za siri ili kuipa ulinzi akaunti yake.

“Tumeamua kuanzisha utaratibu huu ili kuwapa nafasi Watanzania kujivunia mchezo huu ulioanzishwa mahususi kwa watu kushinda na kuimarisha uchumi wao kwa namna moja ama nyingine ikiwa ni mwendelezo wa huduma zetu kama mchezo wetu wa kubashiri matokeo wa bikosports ambao mtandao wa www.bikosports.co.tz unatumika watu kucheza moja kwa moja mtandaoani.

“Mtu mwenye akaunti ya bikoboost ataweza kuweka pesa yake humo ili akiamua kuhamisha pesa wakati anacheza iwe rahisi kwa kiasi kikubwa, tukiamini sasa biko kumenoga,” Alisema Mgeta.
Kuhusu ushindi kwa wanaotumia simu janja na wale wa viswaswadu, Mgeta anasema wote wana nafasi sawa kwa sababu namba zote zinaingia kwenye gurudumu la bahati bila kujali njia inayotumika kucheza Biko.

Anasema pindi mteja atakapoingia kwenye mfumo wao ama kwa kutumia simu ndogo au anayeingia kwa njia ya mtandao wa www.biko.co.tz, basi namba yake itaingia kwenye gurudumu la bahati na kusubiri meseji ya kujipangia ushindi kutoka bikoboost ili aweze kuibuka na dodo la mchezo wa biko.
“Biko ni bahati nasibu ya Watanzania ambapo wote ni mashahidi jinsi watu walivyovuna fedha na wanavyoendelea mpaka sasa, ndio maana kushinda Milioni moja, milioni 5 au hata wanaonyakua milioni 50 kwetu ni kawaida kabisa.

“Badala ya kukaa tu, ni vyema Watanzania wote wakachangamkia fursa ya kujipangia ushindi kutoka kwenye bahati nasibu hii rahisi kucheza na hata ushindi wake unaonekana kwa sababu gurudumu la bahati linazunguuka na kumwaga ushindi kila baada ya dakika moja,” Alisema Mgeta ambaye pia kampuni yao inatoa huduma ya mchezo wa kubashiri matokeo wa michezo mbalimbali wa bikosports ambapo watu wanaweza kucheza live kupitia mtandao wa www.bikosports.co.tz

Watanzania wanaweza kuendelea kunufaika na mchezo wa kubahatisha wa bikoboost na bikosports, ikiwa ni mapinduzi makubwa kupitia huduma ya kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali na kujipatia ushindi na promosheni yao ya Bonge la Site yenye bonansi za kutosha.

Kwa mujibu wa Mgeta, njia zote za kucheza biko ni rahisi zinazotoa ushindi wa papo kwa hapo pamoja na droo kubwa, huku wanaotamani kujua zaidi wakiruhusiwa kuongea na huduma kwa wateja kwa kupiga namba 022220100 ambapo changamoto zozote zinazomkumba Mtanzania juu ya mchezo wa biko zitatuliwa kwa njia rahisi kwa lengo la kuifanikisha fursa hiyo muhimu ya biko na kutoa mwanya wa kila mtu ashinde.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad