HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 18, 2023

Dkt.Rutayuga:Wanafunzi wa Vyuo Vya Ufundi Wakihitimu ni Kwenda Kufanya Kazi

 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu la Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dkt.Adolf  Rutayuga akiwahudumia  wananchi waliotembelea   Banda la NACTVET kwenye Maonesho ya 18 ya Vyuo Vikuu yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

KATIBU Mtenda wa Baraza la Taifa la Elimu na Mafunzo wa Ufundi Stadi (NACTVET) Dkt.Adolf Rutayuga amesema kuwa wanafunzi wanahitimu katika vyuo vya ufundi wanatoka na kwenda kufanya kazi.

Dkt.Rutayuga ameyasema hayo katika banda la NACTVET kwenye maonesho ya 18 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa sifa kubwa ya wahitimu wa vyuo vya ufundi wakihitimu kwenda kufanya kazi ni kutokana na masomo yao ni vitendo zaidi kuliko kukaririshwa kwa nadharia.

Amesema kuwa dunia ya sasa inataka wanafunzi wanapokuwa katika vyuo kuangalia fursa zilizo na changamoto kwenda kutatua kutokana na ujuzi waliopata ambao vyuo vya ufundi vinatoa majibu ya wanafunzi kuwa sehemu ya kutatua changamoto zilizopo.

Dkt Rutayuga amewataka wananchi kutrmbelea banda la NACTVET kupata elimu kuhusia na vyuo vya ufundi.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu la Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dkt.Adolf Rutayuga akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa NACTVET kwenye Maonesho ya 18 ya Vyuo Vikuu yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru (mwenye miwani) akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea Banda la NACTVET kwenye Maonesho ya 18 ya Vyuo Vikuu yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu la Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dkt.Adolf Rutayuga akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru (mwenye miwani) wakati alipotembelea Banda la NACTVET kwenye Maonesho ya 18 ya Vyuo Vikuu yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad