HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 25, 2023

DC TEMEKE AMWAKILISHA RC DAR KUMPOKEA WAZIRI MKUU BURUNDI

Na Mwandishi Wetu

MKUU wa Wilaya ya Temeke Dar es Salaam Mobhare Matinyi amemwakilisha Mkuu wa  Mkoa huo  Albert Chalamila kumpokea Waziri Mkuu wa Burundi, Gervais Ndirakobuca.

Waziri  Mkuu Ndirabobuca amewasili jana Julai 24, 2023 saa 2:15 usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Viongozi wa nchi za Afrika wanakusanyika jijini Dar es Salaam kuhudhuria Mkutano  wa Afrika wa Rasilimali Watu unaofanyika tarehe 25-26 Julai, 2023. Mwenyeji wa mkutano huo ni Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad