Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kigoma tayari kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara leo Julai 26,2023 katika uwanja wa Mwanga Center, Kigoma mjini.
Chongolo akiwa uwanja wa ndege amepokelewa na viongozi mbalimbali wa Chama Chama Mapinduzi na Serikali mkoani Kigoma.
Katika mkutano huo unaotarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya wana CCM pamoja na Wananchi kutoka mkoa huo na Wilaya zake zote na mkoa wa Katavi, Komredi Chongolo na ujumbe wake wataelezea hatua kwa hatua ya uamuzi wa Serikali kuingia makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, lengo likiwa kuhakikisha bandari hiyo inatoa huduma kwa ufanisi mkubwa tofauti na ilivyo sasa.
Katibu Mkuu huyo wa CCM ameambatana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Ndugu Stephen Wassira,Katibu wa NEC Oganaizesheni Usi Gavu,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Ndugu Kitila Mkumbo, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Mhe.Jerry Silaa.
Wednesday, July 26, 2023
Home
Unlabelled
CHONGOLO AWASILI KIGOMA KUTIKISA MKUTANO WA HADHARA LEO.
CHONGOLO AWASILI KIGOMA KUTIKISA MKUTANO WA HADHARA LEO.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment