HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 13, 2023

WAZIRI PROFESA MBARAWA AFUNGUA KIKAO KAZI KATI YA MENEJIMENTI YA WIZARA YA UJENZI NA TAASISI ZAKE JIJINI TANGA

 

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa  akkizungumza wakati akifungua  kikao kazi kati ya Menejimenti ya Wizara (Ujenzi) na Menejimenti za Taasisi zake kinachofanyika kwa siku tatu chenye kauli mbiu ya Kuimarisha ari na morali katika utendaji kazi kilichofanyika Jijini Tanga

Katibu Mkuu Sekta ya Ujenzi Mhandisi Aisha Amour  akizungumza wakati wa kikao kazi hicho

Sehemu ya washiriki wa kikao hicho

Sehemu ya washiriki wa kikao hicho




Na Oscar Assenga, Tanga

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amefungua kikao kazi kati ya Menejimenti ya Wizara (Ujenzi) na Menejimenti za Taasisi zake kinachofanyika kwa siku tatu chenye kauli mbiu ya Kuimarisha ari na morali katika utendaji kazi

Akizungumza wakati wa kikao hicho Waziri Mbarawa amesema uwekezaji ambao Serikali imeingia ubia na Kampuni ya DP ya Nchini Dubai ni jambo lenye maslahi mapana kwa nchi kwa sababu itachangia kuiwezesha Bandari ongezeko la bajeti kwa nchi kutoka asilimia 37 hadi kufikia asilimia 67 kutokana na kwamba itawezesha kuongeza ufanisi mkubwa katika bandari ya Daresalaam.

Waziri Mbarawa alisema mkakati wa Serikali ni kuifanya Bandari ya Dar salaam ifanye kazi kwa ufanisi na mkakati mojawapo ni kuwapelekea kwenye viwango vya kimataifa ili waweze kushirikiana na TPA ili kuweza kuboresha bandari zao.

Aidha alisema miongoni mwa watu ambao wana viwango vya kimataifa ili kuweza kushirikiana na TPA kuboresha bandari zao ni DP World kutokana na kwamba ni kampuni kubwa kati ya makampuni 10 duniani yanayofanya mambo hayo.

Alizitaja kampuni nyengine ni Singapore Ports Authority ,Harshon ya Honkong,DP Word ,MPM sasa ni makampuni hayo makubwa ndio yanafanya kazi hiyo ya kupelekea mizigo na kutoa mizigo na wakaamua kuchukua kampuni uya DP Word .

Alisema wameamua kuchukua kampuni hiyo baada ya kufanya uchambuzi wa kina kwa sababu wanasifa za kipekee ukilinganisha na wengine ya kwanza ni anafanya kazi kwenye bandari sita Afrika ikiwemo kufanya kazi na Bandari 30 ulimwenguni kote lakini wanameli zaidi ya 100 za kuchukulia mzigo duniani.

Aidha alisema kwamba kampuni ya DP Word wana uwezo wa meli nyengine za kuchukulia watalii,kuhamasisha mnyororo mzima wa mizigo toka unapotoka mpaka unafika kwa mteja wa mwisho ikiwemo uwezo wa kujenga bandari kavu maeneo mbalimbali.

“Lakini pia wana uwezo wa kujenga maeneo kwa ajili ya logistiki paki kwa mfano Rwanda wamejenga logistika paki kubwa maana ayke mzigo wa wqafanyabiashara wa Rwanda lazima upitie Dar es Salaam na DRC wana mpango wa kujenga logistic paki kubwa na wenyewe wataweza kuitumia vizuri kupata mzigo mkubwa utakaokwenda Kongo”Alisema

Hata hivyo alisema wakifanya maboresha hayo yataweza kuisaidia Bandari ya Dar kwenye makubaliano watakayoyafanya yamejigawa miradi ya sehemu mbili ambazo ni ya kwanza itaangalia Bandari Dar es Saalaam itaangalia gati namba 1 mpaka 7 wataenda kuangalia gati ya majahazi pamoja na abiria na wataangalia maeneo mawili ya kwanza ni operesheni.

Waziri alisema kwa sababu shida moja ya bandari ya Dar ni wamewekeza karibia trilioni 1 kutoka Gati namba moja mpaka 7 lakini bado utendaji wa kazi hauridhishi kwa sababu hakuna vifaa vya kisasa,miundombinu ikiwemo vifaa vya Tehama vya kisasa sio vizuri.

Hata hivyo alisema kwamba hata utendaji wenyewe wanafanya kazi kwa mazoea hivyo wakimpata DP wanaamini wataona mabadiliko makubwa kwenye Bandari ya Dar hivyo wanawatoa hofu watanzania.

Awali akizungumzia kuhusu kikao hicho alisema kwamba kitachochea utendaji kazi kwa uwazi ikiwemo pamoja na kubuni za kiutendaji zinazolenga kuweka mazingira yenye kuchochea morali kwa watumishi wanaowasimamia.

“Hivyo ni mategemeo yangu kwamba mtakuwa huru katika ,kujadiliana masuala ya kiutendaji kwqa uwazi lengo likiwa kupata mwelekeo mmoja utakaohakikisha wizara na taasisi zake zinatimiza malengo yake vizuri”Alisema

Hata hivyo aliwataka washiriki wa kikao hicho kuhakikisha wanatoa mitazamo yao mbalimbali na wasipofanya hivyo maana ya mkutano huo itakuwa haipo.

Awali akizungumza katika kikao hicho Katibu Mkuu Sekta ya Ujenzi Mhandisi Aisha Amour alisema pamoja na mengine kitakuwa na fursa ya kipekee watendaji kujipanga na kuweka mipango ya kutekeleza malengo waliojiwekea

Alisema sekta ya ujenzi imeendelea kutekeleza majukumu yake katika kuchangia maendeleo ya Taifa kwa kuzingatia viwango vya ubora vya ujenzi na ukaribati wa barabara ,madaraja na nyumba za serikali pamoja na vivuko,ujenzi na upanuzi wa viwanja vya ndege na matengezo ya magari ya serikali.

Katika kutekeleza majukumu hayo leo tumekutana hapa kwa lengo la kuweka mipango na kutafakari nini kifanye ili kuweza kuongeza kasi ya utrekelezajoi wa majukumu yao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad