HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 16, 2023

Garnet Star, Daikin zakubaliana kuuza mashine rafiki kwa mazingira

 

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Daikin India, Bw Toshiharu Surumaru (katikati), akitekeleza moja ya mila na tamaduni za ki Hindi wakati wa ufunguzi rasmi wa showroom ya Daikin katika jengo la Garnet Star Jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto Meneja Mkuu wa Daikin -Biashara za Nje Bw Jayant Jawa na Meneja wa Garnet Star Bw Rajesh Nomulwar.WATANZANIA wamehimizwa kujikita katika matumizi ya bidhaa za viyoyozi ambavyo ni rafiki wa mazingira kwa lengo la kuhifadhi mazingira na wakati huo huo matumizi ya niashati kidogo kupitia bidhaa hizo.


Wito huo umetolewa na Meneja wa kampuni ya Garnet Star Bw Rajesh Nomulwar kusaini mkataba wa ushirikiano katik ya kampuni hiyo na ile ya Daikin. Daikin ni moja wapo ya kampuni zinazoongoza kwa aina bora za viyoyozi duniani.

"Tumechagua kusaini mkataba wa kibiashara na kampuni ya Daikin kwa kuwa ni moja ya makampuni ambazo zinaongoza kwa kuzalisha bidhaa ambazo ni rafiki kwa mazingira na ambazo zinahitajika kwa wingi sana hapa nchini Tanzania”, alisema wakati hafla hiyo amayo pia iliudhuriwa na viongozi wa ngazi ya juu kutoka kampuni ya Daikin.

Bw. Rajesh alisema moja ya sababu ya kampuni ya Garnet kusaini mkataba huo, ni ubunifu uliofanywa na kampuni ya Daikin siku za hivi karibuni pale ilipozalisha aina mpya ya viyoyozi ambzyo ni rafiki kwa mazingira na ambazo zina nishati kidogo.

"Kwa upande wetu, tuna mafundi wenye elimu ya kutosha katika kushughulikia bidhaa hizi mpya, ambao watazingatia ubora wa kimataifa wa kampuni ya Daikin inayozalisha bidhaa hizo”, alisema.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Daikin India-Bw. Toshiharu Tsurumaru na Meneja Mkuu wa Biashara za Nje wakampuni hiyo, Bw. Jayant Jawa waliipongeza kampuni ya Garnet Star kwa hatua iliyopelekea makubaliano hayo ambapo waliahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kampuni ya Garnet Star ili kuhakikisha Watanzania wanapata bidhaa zenye ubora sawa na thamani ya fedha watakazotumia wakati wa kuzinunua.

“Tuna furaha kubwa kuwa sehemu ya Tanzania kibiashara; tumekuwa tukipiga hatua katika kutekeleza majukumu yetu ya kibiashara katika ukanda huu wa Afrika kwa miaka kadhaa sasa”, alisema.

Aliendelea kusema kuwa kampuni ya Daikin imelenga kuwa moja wapo ya kampuni bora za kibiashara katika ukanda wa Afrika Mashariki ifikapo mwaka 2025 na kwamba kampuni hiyo itaendela kujiimarisha katika uwekezaji wa bidhaa ambazo ni rafiki kwa mazingira.

Daikin ni kampuni kutoka Japan ambayo inaongoza katika kuzalisha viyoyozi ambavyo ni rafiki kwa mazingira na ambayo ina kampuni tanzu inayozalisha bidhaa za namna hiyo nchini India.
Viongozi wa kampuni za Daikin na Garnet Star wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi huo.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Daikin India, Bw Toshiharu Surumaru (kulia), Meneja Mkuu wa Daikin -Biashara za Nje Bw Jayant Jawa(katikati) na Meneja wa Garnet Star Bw Rajesh Nomulwar wakionesha moja ya bidhaa za Daikin wakati wa ufunguzi rasmi wa showroom ya Daikin katika jengo la Garnet Star Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad