HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 7, 2023

BALAAAAAA UVCCM ULANGA WAANDAA TAMASHA KUMPONGEZA RAIS SAMIA KWA AJIRA YA VIJANA

 


UMOJA wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM Ulanga unatarajia kufanya tamasha la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa anazozifanya katika kuinua vijana kiuchumi kupitia ajira na utekelezaji wa miradi ya maendeleo

Mwenyekiti wa uvccm wilaya ya Ulanga Shahista Suleman amesema tamasha hilo linatarajia kufanyika juni 10 mwaka huu ikiwa ni katika kumutia moyo Rais kutokana na kazi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya sita kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo hasa katika sekta ya afya, maji, elimu na ajira kwa vijana

Naye katibu wa hamasa na chipukizi wilaya hiyo Thomas machupa amebainisha kuwa pamoja na mambo mengine wanashukuru kwa serikali na mbunge wa jimbo hilo kuwawezesha vijana katika vikundi 7 ambavyo vilipatiwa Pampa za kilimo cha umwagiliaji pamoja na mkopo wa pikipiki 65 kwaajili ya vijana wa bodaboda ndani ya mwaka mmoja tangu viongozi wapya wa UVCCM wilaya hiyo kuingia madarakani

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad