HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 24, 2023

Wananchi mafia wamfagilia Rais Dkt.Samia baada ya kupata jengo la wagonjwa mahututi

 Na Victor Masangu,Mafia

WANANCHI wa Wilaya ya Mafia Mkoa wa Pwani wamemshukuru Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo katika sekta za afya ,elimu,maji na mambo mengine.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ujio wa mbio za Mwenge wa Uhuru ulipowasili Wilayani Mafia kwa ajili ya kutembelea ikiwa sambamba na kukagua, kuzindua,na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo.

Mmoja wa wananchi hao Amina Tuki alisema kwamba ujio wa Mwenge wa Uhuru ni mkombozi mkubwa katika kuchochea kasi ya maendeleo na wananchi kuweza kupata fursa ya kupata huduma za kijamii kwa urahisi.

Aidha alipongeza juhudi zilizofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Mafia kwa kufanikisha mradi wa ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi (ICU) pamoja na jengo la dharura.

"Kwa kweli tunashukuru sana ujio wa Mwenge wa Uhuru umeweza kuja na kutembelea miradi yetu ya maendeleo sisi kwetu imeweza kutusaidia wananchi kutokana na kuwepo kwa huduma ambazo tunazipata kama vile,maji,afya,elimu na mambo mengine muhimu,"alisema

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa AbdalahKaim amewapongeza viongozi wa Wilaya ya Mafia kwa kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo.

Kadhalika kiongozi huyo amewahimiza watendaji na viongozi kuitunza na kuilinda miradi ambayo wameianzisha ikiwa sambamba na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia amebainisha kuwa lengo la Serikali ya awamu ya sita ni kuendekea kuwafikishia huduma za Afya Kwa ukaribu wananchi wake Ili kuondokana na gharama kubwa kwa ajili ya kupata matibabu.

Awali akipokea Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya Ya Mafia Zephania Sumaye amesema mwenge huo utakimbizwa kilomota 99.8 na utatembelea, kuzindua, Kufungua,na kukagua miradi mbali mbali.

Awali akisoma taarifa ya mradi wa jengo la wagonjwa mahututi Mganga Mkuu wilaya amesema Mradi huo umegharimu Kiasi Cha Milioni miatano sitini na nne lengo ikiwa kuboresha huduma za Afya pia majengo haya yatapunguzo vifo visivyo vya lazima kupunguza Gharama za rufaa Kwa Wananch

Naye Mbunge wa Jimbo la Mafia Omary Kipanga amempongeza Rais wa awamu ya sita Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali ya maendeleo na kuahidi kushirikiana bega kwa bega na wananchi wake katika kuwaletea mabadiliko chanya.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad