HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 9, 2023

WADAU WAKUTANA NA KUWEKA MIKAKATI YA KUENDELEZA KILIMO BIASHARA KATIKA KONGAMANO LILILOANDALIWA NA UBALOZI WA UHOLANZI NCHINI

 SEKTA ya kilimo bado inazo fursa mbalimbali ambazo zikitumika ipasavyo zitawezesha uchumi wa nchi kukua sambamba na kuzalisha ajira nyingi kwa watanzania.


Hayo yamebainishwa na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, wakati akifungua kongamano kuwajengea uwezo wakulima kuhusu kilimo biashara lililoandaliwa na ubalozi wa Uholanzi nchini na kufanyika mjini Dodoma, likiwa linawashirikisha wakulima na wadau mbalimbali katika sekta hiyo.

Kwa upande wake,Balozi wa Uholanzi nchini,Mh. Wiebe De Boer, alisema Serikali ya nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania hasa katika sekta hiyo ili izidi kukua na kuongeza uchumi.
Balozi wa Uholanzi nchini, Mh.Wiebe De Boer, akibadilishana mawazo na Waziri wa Kilimo Mh.Hussein Bashe ,muda mfupi kabla ya kuanza kwa kongamano hilo.
Waziri wa Kilimo Mh.Hussein Bashe. akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa wa Uholanzi nchini,Mh.Wiebe De Boer baada ya kufungua kongamano la kuendeleza kilimo biashara nchini.
Wadau wakisikiliza mada wakati wa kongamano hilo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad