HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 29, 2023

WAAKAZI WA MOROGORO WADAIWA KUTUMIA BASTOLA KUIBA SIMU

 
Na Karama Kenyunko 
WAKAZI watatu wa Morogoro Wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  Wakikabiliwa na shtaka moja la unyanganyi wa kutumia silaha na kuiba simu.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo leo Mei 29,2023 na wakili wa serikali Grace Mwanga imewataja washtakiwa hao kuwa ni Sufiani Kideku (30) na Celestine Kamuli (32) wote wanaishi 
Kizuka Morogoro na Hussein Mwinyijuma (41) Mkazi wa Gairo mkoani humo. 

mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Feldnand Kihwonde imedaiwa kuwa, Mei 17, 2023 huko katika eneo la Zaramo mtaa wa Jamuhuri ndani ya Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam washtakiwa waliiba simu moja aina ya iPhone mali ya Hussein Mohamed. 

Imeendelea kudaiwa kuwa washtakiwa mara baada ya wizi huo walimtishia Hussein kwa Pistol aina ya Luger  na kisha kumteka Ili waweze kujipatia fedha.

Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wamerudishwa rumande kwa kuwa makosa ya unyang'anyi wa kutumia silaha hayana dhamana.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 12,2023. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad