HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 25, 2023

TAPSEA YAANZA NA SEMINA KWA MAKATIBU MAHSUSI KUELEKEA MKUTANO WAKE MKUU WA 10, ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Maganga akizungumza wakati ufunguzi wa semina ya siku mbili kwa Makatibu Mahsusi inayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Zanziar (SUZA), mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. Semina hiyo ilitanguliwa na mada mbalimbali za kada hiyo, ikiwa ni kuelekea kwenye Mkutano Mkuu wa kumi wa chama hicho utakaofanyika Mei 26, 2023. Wengine pichani kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti Marcella Komba,  Mkufunzi na Mkuu wa Idara ya Uhazili Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC), Mama Agatha Wanderage pamoja na Katibu wa TAPSEA Anneth Charles Mapima.  
Mkufunzi na Mkuu wa Idara ya Uhazili Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC), Mama Agatha Wanderage akizungumza wakati akiwasilisha mada yake katika semina ya siku mbili kwa Makatibu Mahsusi inayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Zanziar (SUZA), Tunguu mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar Mei 24, 2023. 
Mkurugenzi kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC), Charles Magaya akizungumza wakati akiwasilisha mada yake katika semina ya siku mbili kwa Makatibu Mahsusi inayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Zanziar (SUZA), Tunguu mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar Mei 24, 2023. 
Afisa Elimu Jamii wa Mamlaka ya Kudhiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Queen Komba akizungumza wakati akiwasilisha mada yake katika semina ya siku mbili kwa Makatibu Mahsusi inayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Zanziar (SUZA), Tunguu mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar Mei 24, 2023. 














Sehemu ya Wajumbe wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) wakifatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika siku ya kwanza ya Mkutano wao, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Tunguu, Zanzibar.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad