HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 5, 2023

TAMASHA LA KIJANA JANJARUKA LAZINDULIWA JIJINI DAR, VIJANA WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA

 

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mwanahamis Mkunda akizungumza wakati wa kuzindua tamasha la Kijana Janjaruka litakalofanyika katika Viwanja vya Zakhiem Mbagala jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 20-24, 2023.
Upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Tamamu, James Mgeni akizungumza leo Mei 5, 2023 wakati wa kuzindua Tamasha la Kijana Janjaruka litakalofanyika Mei 20-24, 2023 katika viwanja vya Zakhiem jijini Dar es Salaam.


Wadau mbalimbali wa Tamasha la Kijana Janjaruka wakizungumza leo Mei 5, 2023 wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Kijana Janjaruka litakalofanyika katika Viwanja vya Zakhiem Mbagala jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Mziki wa Utamaduni, Mrisho Mpoto Maarufu kama Mjomba akizungumza leo Mei 5, 2023 wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Kijana Janjaruka litakalofanyika katika Viwanja vya Zakhiem Mbagala jijini Dar es Salaam na kuelezea namna fursa za Mziki zinavyopatikana.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Temeke, Nora Mshiri akizungumza wakati wa kuzindua tamasha la Kijana Janjaruka litakalofanyika katika Viwanja vya Zakhiem Mbagala jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 20-24, 2023.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mwanahamis Mkunda akizungumza wakati wa kuzindua tamasha la Kijana Janjaruka litakalofanyika katika Viwanja vya Zakhiem Mbagala jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 20-24, 2023.

picha za pamoja.

OFISI ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke wakishirikiana na Tamamu waandaa tamasha la Kijana Janjaruka litakalofanyika kwenye Uwanja wa Zakhiem Mbagala jijini Dar es Salaam Kuanzia Mei 20 mpaka 24, 2022.

Mkuu wa Wilaya hiyo Mwanahamis Mkunda akizungumza leo Mei 5, 2023 wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo amesema kuwa lengo la Tamasha hilo ni kuhamasisha Wafanyabiashara na Vijana wote wa Temeke kujiunganisha na biashara pamoja na kupata fursa mbalimbali zilizopo katika wilaya hiyo.

Amesema kuwa Vijana wa Temeke watafahamu fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana katika wilaya ya Temeke, Urahisi wa upatikanaji leseni kwa wafanyabiashara, Kujengewa uwezo na mbinu za kukabiliana na masoko pamoja na kupata burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa hapa nchini.

Amesema kuwa vijana wa Temeke watapanua wigo wa biashara hasa ikizingatiwa kuwa Halmashauri imekuwa ikitenga asilimia 10 ya mapato yake kuwezesha Vikundi vya Maendeleo hususani wanawake, vijana na wenye ulemavu lakini hata hivyo wanufaika wengi wamekuwa na biashara za kujirudia na mazoea kwahiyo ushiriki wa wazalishaji utasaidia sana kuonesha fursa nyingine ambazo vijana wa wanaweza kuzitumia.

Aidha, wadau, Kampuni na wazalishaji mbalimbali wenye kuhitaji mawakala katika Wilaya ya Temeke watatumia vyema Tamasha hili kuwafikia na kuunganisha Wafanyabiashara na Vijana na fursa za bidhaa na huduma wanazozitoa.

Anesema kuwa katika tamasha hilo kutakuwa na programu za mafunzo ya kujiendeleza kibiashara na mbinu za kufikia masoko kwa siku tatu lengo likiwa ni kuwezesha wafanyabiashara wetu kuwa wa kisasa.

"Sambamba na Tamasha hilo, Wilaya inategemea kupokea mwenge wa uhuru siku ya tarehe 24 Mei, 2023 saa mbili asubuhi katika eneo la TAZARA na kumalizia shughuli yetu uwanja wa Zakhiemu, Mbagala."

Licha ya hayo amewaalika Hivyo, wadau wote wa biashara Temeke kushiriki ili kuonesha fursa zilizopo pamoja na wananchi kuja kutembelea ili kujionea na kujipatia fursa hizo adhimu za biashara.

Kwa Upande wa mwakilishi kutoka Tamamu, James Mgeni amesema kuwa maadalizi ya Tamasha la Kijana Janjaruka yanaendelea vizuri.

"Hivyo wadau wa biashara niwahakikishie kuwa Tamasha hili, linaandaliwa kwa weledi na ustadi mkubwa ili kuhakikisha malengo ya kila mdau yanafikiwa, mpaka sasa tunategemea kuwa Tamasha la Janjaruka litatoa fursa zaidi ya 865, kutoa mafunzo mbalimbali kwa vijana zaidi ya 3,500 na watembeleaji zaidi ya 12,200".

Pia amewaalika wadau wote wa biashara wenye fursa mbalimbali kwa Vijana na wafanyabiashara kulitumia vyema Tamasha hilo la Janjaruka ili kuongeza na kupanua wigo wa biashara zao katika halmashauri ya Temeke.

Akizungumzia fursa zitakazopatikana katika Tamasha hilo Msanii wa Mziki wa Utamaduni, Mrisho Mpoto Maarufu kama Mjomba amewaalika Vijana wa Temeke kichangamkia fursa hiyo kwani watashirikiana na wanamziki wengine katika kutoa elimu ya namna ya kutoka kimziki kwa kuwaonyeshea kidole fursa ilipo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad