HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 23, 2023

TAMASHA LA KIJANA JANJARUKA LAFANA, WAJASIRIAMALI, TAASISI MBALIMBALI WACHANGAMKIA FURSA

 

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mwanahamisi, Mkunda akitembelea mabanda kwenye Tamasha la Kijana Janjaruka katika Vuwanja vya Zakhiem, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mwanahamisi, Mkunda akitembelea mabanda kwenye Tamasha la Kijana Janjaruka katika Vuwanja vya Zakhiem, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mwanahamisi, Mkunda akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea mabanda kwenye Tamasha la Kijana Janjaruka katika Vuwanja vya Zakhiem, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tamamu, James Mgeni akizungumza na waandishi wa habari kwenye Tamasha la Kijana Janjaruka katika Vuwanja vya Zakhiem, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Mwanamke Mjasiliamali, Mariam Mtesa akizungumza na waandishi wa habari kwenye Tamasha la Kijana Janjaruka katika Vuwanja vya Zakhiem, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Mjasiliamali mdogo mkazi aa Kibonde maji, Arafa Bofu akizungumza na waandishi wa habari kwenye Tamasha la Kijana Janjaruka katika Vuwanja vya Zakhiem, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Matukio mbalimbali kwenye Tamasha la Kijana Janjaruka.
Picha na Avila Kakingo 


VIJANA wa wilaya ya Temeke waaswa kuchangamkia fursa katika Tamasha la Kijana janjaruka ambalo limekushanya taasisi na kampuni mbalimbali kwaajili ya kutoa elimu ili kila anayefika katika tamasha hilo anufaike.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mei 22, 2023 Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mwanahamisi, Mkunda wakati alipotembelea Tamasha la Kijana Janjaruka katika Vuwanja vya Zakhiem, amesema kuwa fursa nyingi zilizopo ni za vijana na akinamama ili waweze kujiinua kiuchumi.

"Kijana wa Temeke ukishindwa kufanya biashara umeamua mwenyewe."

Amewaaomba vijana kutembelea tamasha hilo ili kuweza kupata elimu mbalimbali kuhusiana na ujasiliamali, mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake na Vijana asilimia sita na asilimia mbili kwa walemavu, pia amesema Benki ya CRDB ipo katika tamasha hilo wakikopesha fedha za biashara kuanzia laki mbili na unarudisha deni ndani ya mwaka mzima na kurudisha bila riba.

Amesema kuwa kwa Wanawake ambao wapo kwenye kikundi wanaweza kuwakopesha kuanzia laki mbili hadi milioni tano halafu wanarudisha mikopo hiyo bila riba ili waweze kujikimu kiuchumi.

Benki ya CRDB Wamekwenda mbali zaidi kwa wanawake wakiwa kwenye kikundi wanakopeshwa kuanzia laki mbili hadi milioni tano, ndugu zangu ukitaka kukaa nyumbani upate masononeko ya moyo ni wewe umeamua." Amesema Mwanahamis

Amesema huduma za matamasha hayo zitasogezwa karibu na wananchi mara kwa mara ili kuhakikisha kwamba wanatemeke na Watanzania kwa ujumla hawakosi taarifa sahihi kihusiana na fursa zilizopo. Amesema tatizo kubwa kwa watanzani namna ya kupata taarifa sahihi.

"Unakutana na mtu ambaye hana taarifa sahihi, akakupa taarifa zisizo sahihi, unajikuta unapata taarifa zisizo sahihi na kupoteza muda mwingi kulalamika kumbe haujapata taarifa sahihi kwaajili ya kuzifanyia kazi."

Pia amewaomba wanatemeke kutumia wiki ya Tamasha la kijana janjaruka kujiandaa na mapokezi ya Mwenge ambao utapokelewa kesho. Mei 24, 2023 katika viwanja vya Tazara jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tamamu, James Mgeni amesema tamasha la Kijana Janjaruka limeanza kuibua hisia za vijana kwenye masuala ya kujitambua, kujiajili, kuajiliwa na kuzijua fursa kwenye maeneo ya kazi.

"Na hili tamasha tumeliandaa kwaajili ya vijana Tanzania nzima ili vijana wajue namna gani wapite ili waweze kujua Tanzania ni nchi yao kwa kuweza kujikwamua kiuchumi na waweze kupambana hali halisi ya kiuchumi iliyopo.

"Tuliandaa tamasha hili ili kuwaleta wafanyabiashara wakubwa, watoa huduma mbalimbali ili vijana wasipate shida sana kutafuta ni wapi pa kupata mikopo na fursa mbalimbali za kupata taarifa sahihi kuhusiana na biashara zao.

Tamasha hilo limekusanya kampuni za Usafiri, taasisi za benki, taasisi zinazotoa huduma mbalimbali kama CRDB Benki, Azania benki, watoa mikopo, UTT Amis na wafanyabiashara wakubwa ili waweze kutengeneza daraja la kuunganisha ili kuwa na mahusiano mazuri.

Amesema katika Tamasha hilo kunawafanyabiasha wanaotafuta mawakala kwahiyo ni fursa kwa vijana kwa watoa fursa hizo katika

Kwa upande wa Mwanamke Mjasiliamali, Mariam Mtesa amesema kuwa wamenufaika na tamasha hilo kwa kupata elimu ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi.

"Mama yeyote yule asisubirie baba akirudi sisi tunao uwezo mkubwa wa kufanya shughuli zetu na tukaweza kujikwamua kiuchumi na familia zetu, mafunzo haya yamenipa funzo kubwa, kuwa mimi sio tegemezi naweza kufanya mambo makubwa.Amesema Mariam

Amewashauri wanawake wanawake wanaodhani wanapoteza muda kwenda kwenye mafunzo, wasikate tamaa kwani hata mbuyu ulianza kama Mchicha, amesema wasikilize mafunzo na kuyafanyia kazi sio kukaa na kupoteza muda.

Mjasiliamali mdogo mkazi aa Kibonde maji, Arafa Bofu ameanza kumshukuru Mungu kuwepo Halmashauri ya Temeke na kupata fursa ya kuhudhuria mafunzo mbalimbali yaliyoandaliwa na Wilaya ya Temeke wakishirikiana na Tamamu katika tamasha la Kijana Janjaruka. Amesema kuwa alikuwa anafanya biashara kiholela leo wamepata fursa ya kupata fursa ya mafunzo hayo pamoja na elimu ya kujiwekea akiba kidogo kidogo.

Amesema elimu waliyoipata itawasaidia katika biashara ndogo ndogo ili kuendeleza katika kuongeza kipato, kutokutumia pesa kiholela.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad