HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 18, 2023

STANDARD CHARTERED YAZINDUA MFUMO WA KIDIGITALI WA STRAIGHT2BANK NEXT GEN

 

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya Standard Chartered Tanzania imezindua rasmi toleo jipya  la mfumo wake wa kibenki wa kidigital uitwao “Straight2Bank Next Gen” ambao  umeundwa ili kukidhi mahitaji ya wateja wa makampuni nchini Tanzania.

Pia Mfumo huo unalenga kuboresha utoaji wa huduma za kibenki kwa haraka na usalama zaidi, na kuwezesha wafanyabiashara  kupata suluhu mbali mbali za kubenki kidijitali.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa tume ya TEHAMA Tanzania, Dk. Nkundwe Moses Mwasaga, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Benki (Transaction Banking wa Standard Chartered) Afrika Mashariki, Makabelo Malumane.

Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Standard Chartered Tanzania, Herman Kasekende na wadau wengine muhimu katika sekta ya benki.Pamoja na uzinduzi wa Straight2Bank Next Gen, benki hiyo pia iliendesha mjadala kuhusu "Umuhimu wa kuelewa urahisi wa kutumia njia mbadala za kibenki kwa wateja."

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Herman Kasekende amesema wanafurahi kuzindua Straight2Bank Next Gen nchini Tanzania, hiyo ni hatua kubwa katika safari yetu ya mageuzi ya kidijitali.

" Sisi kama benki, tumejikita katika utoaji wa suluhu za kiubunifu zinazoendeshwa na teknolojia, ili kukidhi mahitaji ya kila siku ya wateja wetu, na kuhakikisha wanastawi, "amesema na kuongeza benki hiyo imedhamiria kutoa huduma bora za kibenki kwa wafanyabiashara.

Aidha amesema  kuzinduliwa kwa Straight2Bank Next Gen, wanatekeleza ahadi yao huku akieleza wazi Mfumu huo mpya umerahisiha upatikanaji kwa usalama huduma zao  za kibenki ili kusaidia wateja wao kuzingatia kile ambacho ni muhimu zaidi - kukuza biashara zao.

Kwa upande wake, Dk. Nkundwe Moses Mwasaga ambaye ni  Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA  Tanzania,amesema kushuhudi uzinduzi wa Straight2Bank Next Gen, mfumo  ambao utaboresha huduma na kutatua changamoto  za benki kwa wateja hasa wafanyabiashara nchini Tanzania.

" Tunapoendelea kukubali mageuzi ya dijiti katika uchumi wetu, ni muhimu taasisi za kifedha zitumie teknolojia ili kutoa suluhisho za kibunifu ambazo zinakidhi mahitaji."

Straight2Bank Next Gen imeundwa kwa kutumia uzoefu mkubwa wa Standard Chartered wa kidijitali, ili kuwawezesha wateja kupata huduma za kifedha za kidigitali ambazo zinarahisisha ufanyaji wa biashara zao.

Mfumo huo wa kibenki kidijitali wa Straight2Bank Next Gen wa Standard Chartered Tanzania sasa unapatikana kwa wateja wote wa makampuni nchini Tanzania, na benki inahamasisha wateja kuutumia mfumo huo ili  kufikia malengo yao ya biashara.












No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad