HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 15, 2023

Ni haki ya mgonjwa kumshataki daktari anaposhindwa kuridhika na huduma,Daktari afunguka

 


Njombe
MGANGA mkuu wa kituo cha afya Kidugala halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe Dkt,Zedekia Njogela amewakumbusha wauguzi kutoa huduma stahiki kwa wateja ili kuepuka kushtakiwa kwa kuwa mgonjwa anayo haki ya kumfikisha mahakamani daktari baada ya kushindwa kuridhishwa na huduma.

Njogela ameeleza hayo wakati akizungumza na wauguzi wa kituo hicho ambapo amesema ni muhimu kujua na kufanya kazi kwa weledi ili kuepuka changamoto hizo kwa kuwa mgonjwa ana haki ya kupewa kile kinachokusudiwa kutokana na uhitaji wake.

"Mgonjwa ana haki ya kutendewa ambacho anakusudia kupewa kutoka kwa daktari au muuguzi na kama asiporidhika na huduma,anayo nafasi ya kwenda kupeleka shtaka lake mahali atakaposikilizwa,muuguzi ukifanya kazi tofauti utapelekwa Mahakamani"

Amesema endapo itathibitika muuguzi au daktari ameshindwa kutekeleza wajibu wake zipo pia hatua ambazo wizara huchukua ikiwemo kufuta cheti.
Diwani wa kata ya kidugala Wiston Mbilinyi amewapongeza wauguzi wa kituo hicho kutokana na kazi kubwa wanazofanya ndani ya kata hiyo.

"Lazima niwashukuru ninyi wenzetu kwa kazi kubwa mnayoifanya kwasababu hakuna mwanachi wa kata ya kidugala ambaye atasema hajatibiwa na ninyi"amesema Wiston

Atwidike Mgindo ni muuguzi mkuu wa kituo hicho cha afya,kwa niaba ya wauguzi wa kituo hicho amesema wataendelea kutoa huduma bora kwa wananchi huku wakiomba serikali kuendelea kuboresha baadhi ya mahitaji yao iliwaweze kutoa huduma bora zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad