Mkurugenzi wa HEBO Consult, Bulla Boma Hekeno na Rais mpya wa PMI Tanzania Chapter, Wakili Kheri Mbiro wakisaini mikataba ya mashirikiano na Kampuni ya PMI Tanzania Chapter jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2023.Mkurugenzi wa HEBO Consult, Bulla Boma Hekeno na Rais mpya wa PMI Tanzania Chapter, Wakili Kheri Mbiro wakionesha mikataba ya mashirikiano na Kampuni ya PMI Tanzania Chapter jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2023.
Mkurugenzi wa HEBO Consult, Bulla Boma Hekeno akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2023 wakati wa kusaini mkataba wa ushirikiano na kampuni ya PMI Tanzania Chapter ili kuimarisha ujuzi wa usimamizi Miradi nchini kwa ustawi wa uchumi. Kushoto ni Rais mpya wa PMI Tanzania Chapter, Wakili Kheri Mbiro na kulia ni Mkurugenzi wa Ushauri na huduma na Mipango wa HEBO Consult Martin Hekeno.
Kushoto Rais mpya wa PMI Tanzania Chapter, Wakili Kheri Mbiro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2023 wakati wa kusaini mikataba ya mashirikiano na Kampuni ya HEBO Consult
Picha ya pamoja.
KAMPUNI ya HEBO Consult leo Mei 11, 2023 wamesaini Mkataba wa Ushirikiano na kampuni ya PMI Tanzania Chapter katika kutoa mafunzo ya usimamizi wa miradi hapa nchini na Afrika.
Mkurugenzi wa HEBO Consult, Bulla Boma Hekeno akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema kuwa kwa zaidi ya wataalamu wa miradi 500 wamepata mafunzo kwaajili ya kusimamia miradi hapa nchini.
Amesema kuwa wamewezesha upatikanaji wa vyeti vya
kitaaluma vya usimamizi wa miradi karibia 100 na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji na kutambuliwa kwa sekta na taaluma ya usimamizi wa miradi nchini Tanzania na katika Ukanda mzima.
"Ushirikiano huu ulioimarishwa unalenga kuwawezesha wataalamu wa miradi nchini Tanzania kupata ujuzi na maarifa muhimu ili kufanikiwa katika fani yao, huku wakijipatia vyeti vya kitaaluma vinavyotambuliwa kimataifa kama vile PMP (Project Management Professional), kigezo cha juu kwa wasimamizi wa miradi duniani kote tangu kuanzishwa kwa ushirikiano huu mwaka 2021, HEBO Consult imetoa mafunzo." Amesema
Kwa upande wa Rais mpya wa PMI Tanzania Chapter, Wakili Kheri Mbiro akizungumzia umhimu wa ushirikiano huo amesema kuwa ushirikiano wao na HEBO Consult unaimarisha dhamira ya kuwapa wataalamu wa Kitanzania ujuzi wa usimamizi wa miradi, ambao ni muhimu kwa mafanikio ya miradi ya maendeleo ya kitaifa na ukuaji wa uchumi kwa jumla.
Amesema kuwa hivi karibuni, PMI Tanzania itasaini makubaliano ya hiari na serikali ya Zanzibar ili kuanzisha kituo cha ubora wa usimamizi wa miradi, na ushirikiano kama huo na HEBO Consult unawezesha juhudi hizi kuwa na mafanikio makubwa.
"Tunajivunia kuendeleza ushirikiano wetu na PMI Tanzania Chapter, kwani unalingana vizuri na dhamira yetu ya pamoja ya kuwajengea uwezo na kuendeleza wataalamu wa usimamizi wa miradi katika sekta zote ili kuhakikisha mafanikio ya miradi na ukuaji endelevu wa uchumi nchini Tanzania.
Amesema kuwa Wanachama wa PMI Tanzania Chapter wataendelea kunufaika na punguzo la asilimia 20 kwenye mipango yote ya vyeti vya kitaaluma kutoka PMI, pamoja na mafunzo endelevu ya kitaalam kwa wataalamu waliothibitishwa.
Amesema kuwa Ushirikiano huo unaendelea kusaidia katika kuhamasisha mbinu bora za usimamizi wa miradi na kuongeza uelewa wa mipango muhimu ya mafunzo ya usimamizi wa miradi inayojenga wasimamizi wa miradi wenye ufanisi.
No comments:
Post a Comment