Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Zinga Evance Haule akiwatambulisha na kuwakaribisha wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kuwahamasisha wanafunzi hao kujiunga na masomo ya Uhasibu watakapomaliza masomo yao ya Sekondari.
Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA, Magreth Kageya akitoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Zinga iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani.
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Zinga pamoja na kuwahamasisha wanafunzi hao kujiunga na masomo ya Uhasibu watakapomaliza masomo ya Sekondari.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Zinga wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) waliofika kutoa elimu shuleni hapo Bagamoyo mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment