HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 17, 2023

BANK OF AFRICA-TANZANIA YAMZAWADI MSHINDI WA KWANZA WA KAMPENI YAKE YA KIDIGITALI YA 'TRANSACT & WIN'

 Meneja wa Bank of Africa-Tanzania tawi la Mbeya, Agatha Lyimo (Kulia),akikabidhi zawadi ya simu janja kwa Victor Thomas Sowani ambaye ni mshindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya benki hiyo kuhamasisha matumizi ya simu kupata huduma za kibenki inayojulikana kama Fanya Mhamala na ushinde "Transact & Win".iliyofanyika katika tawi hilo jana.

Maofisa wa Bank of Africa-Tanzania wakifuatilia droo ya kupata mshindi wa kampeni ya promosheni ya benki hiyo kuhamasisha matumizi ya simu kupata huduma za kibenki inayojulikana kama Fanya Mhamala na ushinde "Transact & Win"iliyofanyika jijini Dar e s Salaam chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania


KUFUATIA droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kampeni ya Transact & Win iliyofanyika katika ofisi kuu ya BANK OF AFRICA tarehe 11 Mei, 2023, mbele ya Mkaguzi Mwandamizi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Elibariki Sengasenga. Bw. Victor Thomas Sowani, mteja wa BANK OF AFRICA, aliibuka kuwa mshindi wa simu ya I-phone 14 wa kampeni ya kidijitali ya kusisimua ya benki hiyo iliyopewa jina la Fanya Mhamala na ushinde "Transact & Win".

Kampeni ya Transact and Win ilianza tarehe 1 Aprili 2023 na itadumu kwa miezi 3 simu janja za kisasa zitatolewa kwa wateja watakaobahatika kushinda. Wateja wa Bank of Africa wametakiwa kuchangamkia kampeni hii kupitia programu ya kufanya mihamala kidigitali kupitia simu zao za mkononi au programu ya ussd (*150*13#) kufanya miamala mingi iwezekanavyo ili kufuzu kuingia kushiriki katika droo inayofanyika kila mwezi.

Akiongea wakati wa droo hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kidigitali wa BANK OF AFRICA, Bw. Jesse Jackson, alisema kuwa kampeni hiyo inalenga kuwahamasisha wateja wa benki hii kutumia huduma za kidigitali zilizoboreshwa zaidi ili kupata huduma bora kwendana na matakwa yao.

Kampeni hii ni kielelezo cha lengo la kimkakati la benki kuweka bidhaa na huduma zake katika mfumo wa kidijitali na hivyo kukuza ushirikishwaji wa kifedha pamoja na urahisi wa wateja kupata huduma za benki.

Nandi Mwiyombella, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano alisema: “Kupitia kampeni hii hii, wateja wetu na watumiaji wa huduma hii ya B-Mobile katika kipindi hiki cha kampeni wataingia moja kwa moja kwenye droo kubwa ya bahati nasibu pale mteja atakapokuwa amefanya miamala isiyopungua 10 yenye thamani ya TZS 500,000/=.

Bank of Africa tumedhamiria katika kutoa huduma na bidhaa bora zinazokidhi mahitaji ya wateja.” Benki itaendelea kubuni na kuleta mawazo ya kibunifu ili kuendana na kasi ya ukuaji wa tasnia ya benki kidigitali (banking on the Go!!). Hii ni katika kukuza ajenda ya ujumuishaji wa huduma za kifedha." Alisema Bw. Jesse.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad