HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 29, 2023

Aliyempiga mke wake na kumng’oa jino akamatwa

 

Na Mwandishi wetu Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi mkoani Arusha Mei 27, 2023 limefanikiwa kumtamata mtuhumiwa aitwaye Isack Robertson (45) mkazi wa Sombetini Jijini Arusha kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi mke wake aitwaye Jackline Mkonyi (38) mkazi wa Sombetini jijini humo.

Akitoa taarifa hiyo leo Mei 28, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa huko katika maeneo ya Himo mkoani Kilimanjaro na wanaendelea kumhoji na pindi upelelezi utakapokamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.

Aidha ametoa onyo kwa baadhi ya watu wachache wanaofanya vitendo vya ukatili katika familia zao ama sehemu nyingine kuacha mara moja kwani hawatasita kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria.

Lakini pia amewaomba wananchi popote walipo wasifumbie macho vitendo viovu na waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha wanatoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika maeneo yao ili kukomesha matukio hayo katika jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad