Mwandishi wa Chanelten na Radio Magic FM Margaret Malisa akipokea barua ya uteuzi kutoka kwa Katibu wa UWT Kibaha Mjini Mariam Mgasha.



Baadhi ya Viongozi wa UWT Wilaya ya Kibaha wakiwa kwenye Ofisi ya UWT Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.
Na Khadija Kalili, PWANI
UMOJA wa Wanawake Wilaya ya Kibaha Mjini (UWT) wamefanya uteuzi kwa Waandishi wa Habari watatu kutoka Chanel ten na Magic Fm Radio, Margaret Malisa, Diwani wa Viti Maalumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Selina Wilson na Mwandishi wa Magazeti ya Uhuru pamoja na Redio Uhuru Mwamvua Mwinyi kuwa Wajumbe wa Kamati ya Habari na Mawasiliano ya UWT Wilaya ya Kibaha Mjini .
Uteuzi huo una lengo kupanua wigo wa utoaji habari za Chama Cha Mapinduzi (CCM) hususani kutangaza kazi zinazofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ikiwa ni katika kutekeleza ilani ya CCM ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Wilaya ya kibaha Mkoani Pwani.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha Elina Mgonja amesema baada ya kuwakabidhi barua zao za uteuzi huo Wajumbe hao amesema kuwa kuteuliwa kwao kumefanywa Baraza maalumu la dharula la Wajumbe wa UWT Wilaya ya Kibaha.
Mwenyeki huyo amewataka Waandishi hao wa habari kutumia kalamu zao katika kuhabarisha umma mazuri yanayofanywa na CCM katika utekelezaji wa ilani.
" Kamati tendaji tumemua kuwateua hawa Waandishi , ili kuleta nguvu ya pamoja katika kutangaza kazi zinazofanywa na serikali na tunaamin kuwa , watafanya vizuri kwani ni watumishi wa vyombo vinavyomilikiwa na Chama Chetu cha Mapinduzi (CCM) hivyo itakuwa ni rahisi kwao kutangaza kazi zilizofanywa katka utekelezaji wa Ilani ", amesema Mwenyekiti huyo.
Aisha
Baraza hilo pia limepokea taarifa za kazi za Madiwani wa Viti Maalumu, pamoja na kuweka mipango na mikakati ya ushindi wa kishindo mwaka 2024/25.
Mgonja ametumia fursa hiyo kuwataka madiwani kufuata kanuni za baraza la UWT ikiwa ni pamoja na kupeleka taarifa zao za kazi kila baada ya miezi mitatu, kuheshimiana pamoja na kuhudhuria vikao pia kutoa taarifa pindi wanapopata dharula.
Mbali ya Kamati ya Habari na Mawasilano pia Baraza hilo limeunda Kamati zingine ikiwemo ya Kamati ya Uchumi na Fedha , Kamati ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum,
Kamati ya Maendeleo , Kamati ya Afya na Kamati ya Hamasa.
No comments:
Post a Comment