HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 20, 2023

VYUO VIKUU, VYA KATI SABA VYAFIKIWA NA MAFUNZO YA TGNP, INTERNEWS

 VYUO Vikuu na Vya kati saba (7) vya jijini Dar es Salaam vinavyofundisha kozi ya uandishi wa habari vimefikiwa na mafunzo yanatolewa na Mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP) wakishirikiana na Internews.


Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Aprili 20, 2023 Mwenzeshaji kutoka mradi wa Boresha habari unaoratibiwa na Internews, Deogratius Temba amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha wanataaluma hao kuwa na jicho la kijinsia wanapofanya kazi zao hasa za Uandishi, namna ya kuandaa vipindi kutengeneza mabango pamoja na vipeperushi mbalimbali.

“Tumekuwa na program hii ya kutoa mafunzo kwenye vyuo vikuu na vya kati na leo tupo Institute of Arts and Media Communications (IAMCO) ili wajue namna kazi wanazozifanya zinaondoa uzalilishaji, Ukatili wa kijinsia na ukandamizaji katika jamii.” Ameeleza

Ametoa wito kwa wanataaluma hao kutengeneza vipindi na kuandika habari zitakazo badilisha mtazamo wa jamii kwani hata katika masomo yao vipo vipindi vinavyolekeza namna ya kuandika habari zenye kuelimisha jamii na kuwa na jicho la kijinsia zaidi.

Temba ameeleza kuwa mwitikio wa wanataaluma ni mkubwa katika kupata mafunzo hayo kwani elimu wanayoitoa inajenga mjadala mpana zaidi.

Kwa Upande wa Mnufaika wa mafunzo hayo kutoka IAMCO, Nyanzawa Kilima amesema kuwa mafunzo hayo yamemuongezea uelewa na kupanua upeo katika maisha ya kawaida kwani kunamambo anasema alikuwa anayachulia kawaida kuliko uhalisia wake.

“Tunahitaji mijadala mikubwa kuzungumzia suala la ‘jinsi’ ukiachana na mambo ya kuwaempower wanawake na jinsia kwenye jamii kunamambo mengi yanayoendelea yanagandamiza jinsi nyingine na kupendelea nyingine hasa kwenye majukumu katika familia.”

Akizungumzia changamoto iliyopo kwa sasa Nyanzawa amesema kuwa ni malezi ya watoto katika familia na mgawanyo wa majukumu bila kujua hao watoto baadae watakuwa na familia zao.

Ameiomba jamii kubadilisha mtazamo juu ya malezi ya mtoto kuwa ni ya mama tuu, malezi ya watoto ni ya baba na mama amesema kuwa mama peke yake hawezi kufanyikisha hayo bila kuwa na mitazamo chanya juu ya malezi ya watoto.

Kwa upande wa Mkufunzi wa Kamera, AIMCO, Ombeni Mbwambo amesema kuwa upigaji picha zenye mrengo wa kijinsia ni mhimu kwani picha zitakazo pigwa haziendi kumdhalilisha aliyepigwa picha hiyo.

“Siku hizi kumekuwa na mtindo wa kupiga picha zinazodhalilisha utu wa mtu, hasa akinamama na akinadada mengi tumeona kwenye matangazo mbalimbali pamoja na mabango yanakuwa hayana jicho la kijinsia.” Ameeleza Mbwambo.

Amesema kuwa leo wameelekezwa namna ya kuandika habari zinazohusu mambo ya kijinsia, kunatofauti ya kurepoti habari ya mwanamke pamoja na mwanaume utofauti uliopo hasa ni kwenyeushawishi wa mwanamke na mwanaume kutoa habari, ametolea mfano kwa mwanamke au mwanamke aliyefanyiwa ukatili wa kijinsia ni tofauti hata upigaji wake wa picha.
Mwenzeshaji kutoka mradi wa Boresha habari unaoratibiwa na Internews, Deogratius Temba  akizungumza na wanafunzi wa Institute of Arts and Media Communications (IAMCO) jijini Dar es Salaam leo Aprili 20, 2023.
Mwenzeshaji kutoka mradi wa Boresha habari unaoratibiwa na Internews, Deogratius Temba akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mafunzo katika Institute of Arts and Media Communications (IAMCO) jijini Dar es Salaam leo Aprili 20, 2023.
Mkufunzi wa Kamera, AIMCO, Ombeni Mbwambo akichangia maa jijini Dar es Salaam leo Aprili 20, 2023 wakati wa mafunzo ya TGNP na Internews kupitia mradi wa Boresha habari.
Mnufaika wa mafunzo hayo kutoka IAMCO, Nyanzawa Kilima akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili 20, 2023.
Matukio mbalimbali wanafunzi wakisikiliza mada leo Aprili 20, 2023.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad