HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 27, 2023

TUZO 52 KUPAMBA USIKU WA TMA

 


Na.Khadija Seif, Michuzi TV
WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Pindi Chana anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha Usiku wa Tuzo za muziki (TMA) Aprili 29,2023 Ukumbi wa Superdome Masaki Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Wanahabari Leo Aprili 27,2023 Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Dkt.Kedmon Mapana amesema mchakato wa tuzo ulizunduliwa rasmi mapema mwezi Februari 2023 na ukawataka wasanii kupendekeza kazi zao ziingie kwenye Kinyang'anyiro hicho cha tuzo kwa mwaka 2023.

"Wasanii wengi waliojitokeza kupendekeza kazi zao ambapo kwa mwaka 2023 zaidi ya Kazi 1700 ziliweza kukusanywa ."

Hata hivyo Mapana amesema Usiku huo ni mahususi kwa watu mahiri zaidi pia akaongeza kuwa jumla ya tuzo 52 zitatolewa siku hiyo.

"Tutakuwa na vyeti vya taasisi ambazo zimekuwa zikitoa mchango mkubwa katika muziki pia Usiku huo watatambuliwa pamoja na wasanii ambao wataibuka washindi kwenye vipengele vya tuzo watapatiwa tuzo zao."

Aidha Mapana amewaambia wasanii na wadau wa Sanaa kujitokeza kwa wingi mapema Aprili 28,2023 katika ukumbi wa "Superdome" kwa ajili ya Semina kuelekea Kilele cha Usiku wa tuzo hizo.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa Dkt.Kedmon Mapana akizungumza na Wanahabari leo Aprili 27,2023 kutoa taarifa rasmi ya maandalizi ya Usiku wa Tuzo za muziki nchini (TMA) zinazotarajiwa kufanyika Aprili 29,20223  Ukumbi wa Superdome Masaki Jijini Dar es salaam huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo  Dkt.Pindi Chana

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad