KITUO cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimezindua jukwaa la Majadiliano ya vijana ndani vyama vya Siasa jijini Dar Es Salaam leo Aprili 19, 2023, viongozi wa vyama waomba kufungua milango ili vijana washiriki kikamilifu.
Makamu Mwenyekiti wa TCD na Manachama wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jukwaa hilo, amesema kutokana na kuwa na malengo ya muda mrefu ya kuwa na jukwaa la vijana, sasa wamezindua ili kuwapa fursa vijana kujadili na kubadilishana mawazo katika ushiriki wao kwenye vyama vyao vya siasa.
Amesema jukwaa hilo litaweza kuwasaidia vijana kujenga uwezo wao wa kiuongozi kwani TCD inaamini kuwa vijana ndio viongozi wa leo.
Amesema kuwa hata kwenye takwimu za Sensa ianaonesha kuwa vijana ni wengi ni zaidi ya kuliko makundi mengine ya watanzania wote kwa hiyo ni muhimu kushiriki katika uongozi wakiwa bado na nguvu ili kueza kuleta maendeleo katika siasa, vyama vyao na nchi kwa ujumla.
"Masuala ya maendeleo ni masuala yanayowagusa sana vijana, Elimu bora, Masuala ya haki, ajira na Uwezeshwaji, kupata huduma bora za afya yote ni masuala ya vijana na ndio watakaoishi miaka mingi itakayokuja."Amesema Lipumba
Kwa Upande wa Mkurugenzi wa TCD, Bernadetha Kafuko amewaomba Viongozi wa Vyama vya siasa wafungue milango ili kuhakikisha jitihada mbalimbali zinazofanywa na wadau katika kuhakikisha vijana wanashiriki katika kwenye nafasi mbalimbali za maamuzi zinazaa matunda.
“Vyama Mfungue Milango msiseme siku zote hawa bado wadubiri kesho, hawa ndio viongozi wa leo, kiongozi wa kesho tuanze kumuandaa leo kwa kukaa nae mezani kumwonesha jinsi gani tutunafanya maamuzi ya nchi.
Hata hivyo aliwaomba vijana kuonesha uwezo ili kuweza kupata nafasi ya uongozi kwenye vyama vya siasa.
Licha ya hayo amewataka vijana kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Wadau mbalimbali wanaohakikisha vijana wanapata siti kwenye meza za maamuzi katika vyama vyao vya siasa.
Kwa Upande wa Wawakilishi wa Vijana, John Pambalu na Rehema Sombi wakizungumzia wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo, wameeleza kwawa litawawezesha kukaa pamoja na kujadiliana mbinu mbalimbali za kisiasa ikiwemo matumizi ya Tehama katika shughuli za kisiasa.
Makamu Mwenyekiti wa TCD na Manachama wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza wakati wa uzinduzi wa jukwaa la Majadiliano ya Vijana ndani ya vyama vya siasa jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 223.
Kiongozi wa Chaumma, Hashimu Rungwe akizungumza na baadhi ya vujana wakati wa uzinduzi wa jukwaa la Majadiliano ya Vijana ndani ya vyama vya siasa jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 223.
Picha za Pamoja wakati wa uzinduzi wa jukwaa la Majadiliano ya Vijana ndani ya vyama vya siasa jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 223.
Matukio mbalimbali.
No comments:
Post a Comment