HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 25, 2023

TCD WAASWA KUITAFAKARI RIPOTI WAKIWA NA JICHO LA KIJINSIA

 

Msajili wa vyama vya Siasa Jaji Francis  Mutungi akizungumza wakati wa kufungua mjadala wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD)  jijini Dar es Salaam leo Aprili 25, 2023 wakati walipokuwa wakijadili ripoti ya maprngo ya kijinsia katika nyaraka za kisera za vyama vya siaa nchini.
Makamu Mwenyekiti wa TCD na Manachama wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza wakati walipokuwa wakijadili ripoti ya maprngo ya kijinsia katika nyaraka za kisera za vyama vya siaa nchini  jijini Dar es Salaam leo Aprili 25, 2023.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
MSAJILI wa vyama vya Siasa Jaji Francis  Mutungi ametoa wito kwa Vyama vya siasa kuitafakari repoti na kufanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa kwenye ripoti ya uchambuzi wa mapengo ya kijinsia katika nyaraka za kisera za vyama vya siasa kwani wanawake wanastahili na wanahaki sawa ya kukaa kwenye meza za maamuzi katika ngazi zote.

Ameyasema hayo leo Aprili 25, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mjadala wa kupitia ripoti ya uchambuzi wa mapengo ya kijinsia katika nyaraka za kisera za vyama vya siasa hapa nchini. Amesema kuwa Ushiriki wa Wanawake ni mhimu kwa kujenga jamii yenye ushiriki huku vyama vya siasa ndivyo vilivyoshikilia geti la uongozi nchini ndio wanaoamua nani aingine na nani asiingie kwenye uongozi.

Pia amesema lazima kuwe na utashi wa wadau wa siasa kwaajili ya kumsaidia yule ambaye anastahili kwa lengo la kuweka usawa wa mfumo ambao utasababisha uwiano wa kijinsia katika vyama.

"…Lazima kuwe na mkakati wa makusudi ili kukuza uzoefu na uelewa wa kijinsia isije kuwa tunataka kuweka uwiano wa kijinsia halafu mantiki ya ile nafasi ya uongozi tukaiweka pembeni, haitaleta maana." Amesema Jaji Mutungi

Wakati huo huo amewaomba Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kumaanisha kile wanachokijadili leo kwasababu anataarifa ya misuguano ndani ya vyama vya siasa kati ya wanawake na wanaume.

Amesema kuwa ushiriki wa wanawake katika nafasi za meza za maamuzi bado ni ndogo ikilinganishwa na kiwango kilichopo sasa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na mapendekezo yaliyotolewa kwenye sheria ya vyama vya siasa toleo la mwaka 2019 iliagiza vyama vya siasa kuzingatia misingi ya jinsia katika miundo na mifumo ya uendeshaji wa vyama hivyo.

”Vyama vya siasa ndio taasisi zenye fursa ya kutoa viongozi wa kisiasa hivyo ni mhimu kwa misingi na taratibu zinazozingatia misingi ya mbalimbali ya wanajamii katika nafasi mbalimbali za uongozi kwani katiba inatoa haki kwa raia yeyote wa kuanzia miaka 21 kugombea nafasi mbalimbali za uongozi pia sheria ya vyama vya siasa inatoa haki kwa makundi mbalimbali kushiriki katika shughuli za kisiasa." Ameeleza

Aidha ametambua mchango wa wanawake kwenye vyama vya siasa kwa hamasa ya kusimamia shughuli za vyama vya siasa nyakati zote hususani nyakati za uchaguzi.

Kwa Upande wa Makamu Mwenyekiti wa TCD na Manachama wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema kuwa ushiriki wa wanawake ni mhimu kwani wanapaswa kuwa viongozi.

Akizungumzia kuhusu idadi ya watu Prof. Lipumba amesema kuwa idadi ya wananwake ni kubwa ukilinganisha na idadi ya wananume na hata wapiga kura wengi ni wanawake lakini wawakilishi katika nafasi mbalimbali za uwakilishi na uongozi ni wachache.

Akielezea takwimu za uwakilishi wa uongozi katika nchi na mabunge Prof. Lipumba amesema kuwa nchi inayoongoza kati ya nchi 192 duniani ni Rwanda ambayo inawabunge wanawake asilimia 61.03 ingawa nchi hiyo sio nchi ya kidemokrasia na Tanzania tunashika nafasi ya 34 kati ya nchi 192 zenye wawakilishi wanawake katika ngazi za maamuzi.

“Kikao hiki ni mhimu lakini tunajadili ushiriki wa Wanawake huku tukijenga mifumo ya demokrasia…… kwahiyo tunahitaji tuwe na ushiriki ndani ya vyama ndani ya nchi ndani ya serikali lakini tuwe na mfumo wa kidemokrasia.” Ameeleza

Kwa Upande wa Mkurugenzi wa TCD, Bernadetha Kafuko akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa TCD na Manachama wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema kuwa lengo la kukutana leo ni TCD kufanya mapitio ya kwenye nyaraka mbalimbali za vyama katika kuangalia mapungufu ya kijinsia yaliyopo kwenye nyaraka za kisera za vyama vya siasa.

Amesema kuwa baada ya kufanya mapitio ya nyaraka hizo watazingatia mapendekezo yatakayosaidia kuongeza ushiriki wa wanawake katika vyama na sio tuu kama wasindikizaji lakini washiriki kama viongozi na washiriki kama viongozi na waweze kukaa kwenye meza za maamuzi.

Amesema kuwa vyama vitano ambavyo ni wanachama wa TCD watafanya mapitio hayo vyama hivyo ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ACT Wazalendo, CUF na chama cha NCCR Mageuzi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad