HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 17, 2023

NHC YAANZA UJENZI WA MRADI WA ZAIDI YA BILIONI MOJA KAHAMA

 

Mbunifu Majenzi (Arch)  Robert Kintu wa NHC (aliyenyoosha kidole) akimwelekeza jambo Injinia Mburuga Matamwe (mwenye shati la dtaft) na Godfrey Mkumbo (kushoto) na Mhandisi Masumbuko Majaliwa,  wakiangalia ramani ya maduka hayo.
Mbunifu Majenzi, Robert Kintu kutoka Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) akiangalia mchoro na Wataalamu Wengine.

Na Mwandishi Wetu, Kahama
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi kwa Mkandarasi wa Shirika eneo kunatakapoaza kujengwa majengo ya kitega uchumi yakiwamo maduka, supermarkets, maeneo ya kuoshea magari na maeneo ya huduma mbalimbali za kijamii.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari, Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Shinyanga, Angelina Magazi amesema mradi huo unajengwa ili kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara wilayani humo.

Amesema kuwa mradi huo utakapokamilika utagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja za Kitanzania.

Naye Mshauri wa Mradi huo, Godfrey Mkumbo amesema ujenzi wa majengo hayo ya kisasa utakamilika ndani ya miezi sita ukiwa umezingatia viwango vya kisasa.

Amesema mradi huo utakuwa na jumla ya maduka 54 yakiwa na huduma zote muhimu za supermarkets, migahawa na maeneo ya kuoshea magari.

Mradi huo unajengwa kwenye eneo la Bukondamoyo mjini Kahama, Shinyanga ilipo stendi mpya ya mabasi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad