HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 5, 2023

Msukumo wa Rais Samia Sekta ya Madini, Wachangia Trilioni 1. 19 Madini ya Viwandani

 *Waziri Biteko ataka wenye Viwanda kununua Madini kwa bei Elekezi, watakiwa kuwasikiliza wadau

*Awasisitiza Wachimbaji Wadogo kuzalisha madini yenye ubora kuepusha hasara
*Azindua Kalenda ya Mafunzo kwa Wachimbaji Wadogo, ashuhudia utiaji saini makubaliano kati ya STAMICO, taasisi za fedha na wauzaji wa vifaa vya uchimbaji
*STAMICO kuwafikia wachimbaji wa Chumvi, Vito
*Asteria Muhozya na Bibiana Ndumbaro- Dar es Salaam

IMEELEZWA kuwa msukumo uliowekwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu katika Sekta ya Madini umewezesha kuongeza kasi ya ukuaji wa sekta ndogo ya madini ya Viwandani ambapo katika kipindi cha miaka miwili madarakani, mchango wa madini hayo umefikia shilingi Trilioni 1 na bilioni 19 kutoka milioni 451.6.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko wakati akifungua mkutano wa Siku mbili wa Wachimbaji wadogo na wadau wa Madini ya Viwandani ulioandaliwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kushirikiana na Chama Cha Wachimbaji Wadogo Mikoa ya Dar es Salaama na Pwani na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI).

Akizungumza katika ufunguzi, Waziri Biteko amewataka wamiliki wa viwanda kuhakikisha wananunua madini hayo kutokana na bei elekezi iliyowekwa na Serikali huku akiwataka wachimbaji wadogo wa madini hayo kuzalisha madini yenye ubora ili kuepusha hasara kwa wenye viwanda.

Katika hatua nyingine, ameitaka makubaliano yaliyowekwa kati ya STAMICO, taasisi za fedha na wauzaji wa vifaa za uchimbaji madini kutoa matokeo chanya kwa kuwa wajibu wa kuwalea wachimbaji wadogo si hisani bali takwa la kisheria.

Akizungumzia mchango wa wachimbaji wadogo, kwenye maduhuli ya Serikali amesema yamefikia asilimia 40 kutoka asilimia 4 na na kutaka watu wenye ulemavu na wanawake kuchangamkia fursa zilizopo kwenye sekta ya madini ili wasibaki nyuma.

Aidha, amepongeza juhudi zilizofanywa na STAMICO kuwafikia wachimbaji mbalimbali na kusema kwamba viwanda vinahitaji maligafi hivyo, mikutano kama hiyo itawezesha ukuzaji wa viwanda nchini kupitia sekta ya madini.
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akizungumza wakati kufungua mkutano wa Siku mbili wa Wachimbaji wadogo na wadau wa Madini ya Viwandani ulioandaliwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akizindua Kalenda ya Mafunzo kwa Wachimbaji Wadogo na kushuhudia Utiaji Saini Makubaliano ya kuwasaidia wachimbaji wadogo baina ya STAMICO na Taasisi za Fedha na Wauzaji wa Vifaa vya uchimbaji ili kuweza kuwasaidia wachimbaji wadogo.

Matukio Mbalimbali katika Mkutano wa Wachimbaji Wadogo wa Madini na Wadau wa Madini ya Viwandani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad