HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 28, 2023

JESHI LA POLISI LIMEKAMATA WATUHUMIWA 132 MKOANI SHINYANGA

 






Na Elias Gamaya Shinyanga
JESHI la polisi mkoa wa Shinyanga kupitia kitengo cha upeleleze kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia machi 22,2023 hadi aprili 26,2023 limefanikiwa kukamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa 132 katika kesi 129 zilizolipotiwa kwa kipindi cha mwezi mmoja

Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema mpaka sasa kesi zilizopata mafanikio ni kesi 62 miongoni kwa kesi hizo ni pamoja na makosa ya ukatili wa kijinsia, mimba kwa wanafunzi kesi 04, kubaka kesi 02 na kulawiti kesi 01 ikiwemo ni pamoja na watuhumiwa kufungwa jela kifungo cha nje pamoja na kulipa faini

Kwa upande mwingine kamanda Magomi amesema kwa kipindi cha mwezi mmoja pia jeshi la polisi limefanikiwa kukamata bunduki 05 ambazo zilikuwa zikimilikiwa kinyume cha utaratibu wa sheria bunduki hizo ni MARK IV yenye namba Tz car 89939 na risasi 04, MARK IV yenye K 9239 na risasi 03, MARK IV yenye namba D 6,000 na risasi 01 na MARK IV yenye namba MG 564884 na silaha nyingine ni Short gun Birmingham England na risasi 01.

Kamanda Magomi ameongeza kua kwa kipindi cha mwezi mmoja wamefanikiwa kukamata vitu na vielelezo mbalimbali ikiweno pikipiki 06,pombe ya moshi lita 120 vifaa vya kupiga ramli chonganishi,vipodozi vyenye viambata vya sumu ambavyo haviruhusiwi kwa matumizi ya binadamu, pombe kali aina ya Hakiri boksi 12,na bidhaa mbalimbali zilizoibiwa kutoka kwenye maduka mabimbali.

Aidha Jeshi la polisi mkoani Shinyanga linaendelea kuwaasa wananchi kufuata sheria za nchi wakati wote na kutojihusisha na vitendo vya kihalifu kwa namna yoyote na kutoa taarifa dhidi ya vitendo hivyo miongoni mwa jamii inayowazunguka na jeshi la polisi mkoani humo halitakuwa na muhali kwa yeyote atakae jihusisha na vitendo ya kihaLifu.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad