Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa William Mwegoha wakati wa uzinduzi Kamati ya Ushauri wa Viwanda leo Aprili 24 jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuangalia mambo mbalimbali hapa nchini ili kuinua uchumi.
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza wakati wa kuzindua Kamati ya Ushauri wa Viwanda leo Aprili 24 jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuangalia mambo mbalimbali hapa nchini ili kuinua uchumi.
Baadhi ya wanakamati ya Viwanda wakiwa katika uzinduzi Kamati ya Ushauri wa Viwanda leo Aprili 24 jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuangalia mambo mbalimbali hapa nchini ili kuinua uchumi.
Picha ya pamoja.
KATIKA kutekeleza Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi yaani (Higher Education for Economic Transformation [HEET] project) unaofadhiliwa na benki ya Dunia Chuo Kikuu Mzumbe wazindua Kamati ya Ushauri wa Viwanda leo Aprili 24 jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuangalia mambo mbalimbali hapa nchini ili kuinua uchumi.
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza wakati wa kuzindua kamati hiyo amesema kuwa kamati hiyo itaangalia mahusiano yapoje kati ya mazao yanayotoka katika taasisi za elimu ya juu na Viwanda vyetu hapa nchini.
Wanafunzi wanatoka katika vyuo vyetu hapa nchini wanaendana na mahitaji yanayohitajika sokoni hasa kwenye viwanda vyetu apa nchini.
Amesema kuwa kumekuwa na kilio cha muda mrefu juu mahitaji ya soko ni tofauti na wanaozalishwa kutoka kwenye vyuo vyetu yaali wahitimu hawaendani na soko la ajira lililopo.
“Kuzinduliwa kwa kamati hii sasa kunakwenda kuiangalia kwa kina changamoto hii ambayo imekuwepo kwa muda mrefu kati ya waajiri na waajiriwa.
Tunaamini tunakwenda kulifikia lengo kujibu changamoto hii ili kama tatizo lipo kwenye mitaala yetu tushughulike na mitaala ambayo italingana na mhitaji mhimu sokoni."
Akizungumzia kuhusiana na changamoto zilizopo kati ya waajiri na waajiriwa amesema kuwa taasisi ya waajiri Tanzania (ATE)wamewahi kufanya utafiti mwaka 2011 hadi 2014 juu ya wakaja na una ushauri kuwa mazao ya taasisi za elimu za juu haziendani na soko la Ajira lililopo hasa viwandani.
“Lakini hata kwenye vikao tunavyokaa na sekta binafsi nao wanalalamika kuwa wanapowachukua wafanyakazi kutoka vyuo mbalimbali wanalazimika kwenda kuwapa mafunzo nje ya nchi ndio waje wafanye kazi waliyokusudiwa.” Ameeleza
Kwa Upande wa Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa William Mwegoha amesema chuo hicho kimepewa dola za Marekani Milioni 21 ili kutekeleza mradi huo, asilimia 80 na fedha hizo ni kwaajili ya ujenzi wa miundombinu na asilimia 20 ni kwaajili ya kutekeleza mambo mengine ikiwemo kuendeleza wanataaluma.
Amesema kuwa Katika mradi huo wataanzisha mbinu bunifu za kufundishia ikiwa ni pamoja na kuboresha mitaala ya kufundishia na kujenga ushirikiano na Sekta ya viwanda pia kuwa na atamizi ya kuwanoa wataalamu mbalimbali watakaoenda kufanya kazi katika viwanda hapa nchini.
“Ili kutatua changamoto ya ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko na uchumi wa sasa kwa wahitimu wetu, sisi Chuo Kikuu Mzumbe kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), tumedhamiria kujenga muunganiko imara katika ya elimu ya juu na viwanda. Kupitia mradi huu tunatazamia kuwa tutajenga mashirikiano, ubia, na kuendesha shughuli za pamoja na viwanda ambazo zitawawezesha wanafunzi na wafanyakazi kupata ujuzi na uzoefu kupitia kushughulika na changamoto halisi zinazotokea katika viwanda na soko la ajira.” Amesema Prof. Mwegoha
Kwa upande wa mwakilishi wa Wanafunzi na Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe, amesema kuwa wataenda kuyafanyia kazi maelekezo waliyopewa ikiwa ni pamoja na kujifunza kwa bidi ili kuendeleza taifa kwa vitendo.
Mradi huo unatekelezwa nchini kupitia Wizara ya Elimu sayansi na Teknlojia hapa nchini kwa upande wa Chuo kikuu Mzumbe, Kamati hiyo ya Ushauri wa Viwanda ni moja ya eneo la utekelezaji katika mradi huo ukiwa na malengo ya kujenga muunganiko mzuri na imara kati Chuo Kikuu Mzumbe na Sekta ya Viwanda katika kutoa ushauri na kushirikisha uzoefu juu ya maendeleo ya viwanda, mchango wa Elimu ya Juu katika viwanda na ukuaji wa uchumi nchini.
Kutoa mchango stahiki katika utekelezaji wa mpango mkakati wa Chuo Kikuu Mzumbe na kutoa mchango stahiki juu ya fursa za ajira, mentorship, na mafunzo kwa wanafunzi na wafanyankazi kwa vitendo kupitia mashirikiano mazuri kati ya Chuo Kikuu na Mzumbe na Sekta ya viwanda.
No comments:
Post a Comment