HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 6, 2023

22 WAHITIMU MAFUNZO YA USAFIRISHAJI KWA NJIA YA MAJI NIT

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Kaimu Mkeyenge akiwatunuku vyeti Wahitimu 22 kutoka nchini Kenya wa kozi ya muda mfupi ya Cargo tallying for international shipping inayohusika na kuhudumia shehena ndani na nje ya nchi kwenye Mahafali ya kwanza ya wahitimu wa kozi hiyo ambayo yamefanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo Aprili 6, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Kaimu Mkeyenge na Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Prof. Zacharia Mganilwa wakiwa katika picha za ya pamoja na wahitimu 22 kutoka nchini Kenya wa kozi ya muda mfupi ya Cargo tallying for international shipping inayohusika na kuhudumia shehena ndani na nje ya nchi. Hafla ya kuwatunuku vyeti wahitimu hao imefanyika leo Aprili 6,2023 NIT Jijini Dar es Salaam.


CHUO Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimewatunuku vyeti wahitimu 22 kutoka nchini Kenya wa kozi ya muda mfupi ya Cargo tallyingi for international shipping inayohusika na kuhudumia shehena ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwatunuku vyeti wahitimu hao, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Kaimu Mkeyenge amesema, Sekta ya Usafirishaji kwa njia ya Maji umepiga hatua katika Ukanda wa Afrika Mashariki hivyo amewataka vijana kuchangamkia fursa hiyo kwa kusoma kozi za kuhakiki Shehena zinapotoka na kuingia nchini.

Sekta hii imepiga hatua katika ukanda wa Afrika Mashariki hivyo ni Muhimu kuwa na wataalamu wa kutosha watakaokuwa na uwezo mathubuti wa kuhudumia eneo hilo.

Amesema kuwa madhumuni ya kozi hiyo fupi ni kuwajenga vijana kuwa wahakiki wazuri wa shehena zinazotoka nchi za nje kuingia ndani ya nchi za Afrika Mashariki ikiwa pamoja na zile zinazotoka nchini kwenda nchi nyingine kwa kupitia vyombo vya usafiri kwa njia ya maji.

“Hii ni moja ya mpango wa kubadilishana wakufunzi na wanafunzi katika eneo la kanda ya Afrika Masharikii ni katika kutekeleza mradi unaendeshwa na benki ya dunia katika vyuo vilvyopo katika kanda yetu.".

Amesema kuwa kozi hiyo ya mwezi mmoja ina kwenda kuwafanya kuwa wafanyakazi wazuri katika maeneo ya bandari na uingizwaji na utolewaji wa shehena lakini pia katika maeneo ambayo ufungwaji wa shehena unafanyika katika maeneo ya bandari.

Aidha Mkeyenge amesema kuwa wanafunzi wengine wanatarajiwa kupokelewa kwajili ya kubadillishana uzoefu na mafunzo huku na wanafunzi wa hapa nchini wataenda katika vyuo vya nchi nyingine kwaajili ya mafunzo hayo.

Amesema kuwa ushirikiano huo unasaidia kukuza uchumi wa kikanda kupitia njia ya usafiri kwa njia ya maji pia ushirikiano huo utawezesha kufanya biashara za kikanda bila kutegemea nchi nyingine.

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Profesa Zacharia Mganilwa amesema kuhitimu ya wanafunzi hao 22 ni zao la kwanza tangu kuanzishwa kwa kituo cha umahari wa usafiri wa anga na Operesheni za usafirishaji chuoni hapo.

Amesema katika mradi wa benki ya dunia vituo vya Umahiri vipo 16, kwa Tanzania vipo vinne ikiwa kimojawapo kipo NIT ambacho kimewatunuku vyeti vyao wahitimu 22 kutoka nchini Kenya.

Kwa nchini Kenye vituo vya umahili vipo vitano na Ethiopia vipo vituo sita (7) ambavyo vinawezesha wakufunzi na wanafunzi kubadilisha ujuzi na mbinu za ufundishaji.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake mhitimu, Victor Omondi waliohitimu mafunzo hayo ya mwezi mmoja kutoka Chuo cha Kenya Coast National Polytechnic (KCNP) Mombasa amesema ushirikiano huo ni muhimu katika kuendeleza taaluma na ujuzi wa wanafunzi katika vyuo vinavyonufaika na ufadhili huo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Kaimu Mkeyenge akiwatunuku vyeti Wahitimu 22 kutoka nchini Kenya wa kozi ya muda mfupi ya Cargo tallying for international shipping inayohusika na kuhudumia shehena ndani na nje ya nchi kwenye Mahafali ya kwanza ya wahitimu wa kozi hiyo ambayo yamefanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo Aprili 6, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Kaimu Mkeyenge akizungumza wakati wa Mahafali ya kwanza ya Wahitimu 22 kutoka nchini Kenya wa kozi ya muda mfupi ya Cargo tallying for international shipping inayohusika na kuhudumia shehena ndani na nje ya nchi ambayo yamefanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo Aprili 6, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Prof. Zacharia Mganilwa akizungumza wakati Mahafali kwanza ya Wahitimu 22 kutoka nchini Kenya wa kozi ya muda mfupi ya Cargo tallying for international shipping inayohusika na kuhudumia shehena ndani na nje ya nchi ambayo yamefanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo Aprili 6,2023 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia Mahafali ya Wahitimu 22 kutoka nchini Kenya wa kozi ya muda mfupi ya Cargo tallying for international shipping inayohusika na kuhudumia shehena ndani na nje ya nchi ambayo yamefanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo Aprili 6, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu 22 kutoka nchini Kenya wa kozi ya muda mfupi ya Cargo tallying for international shipping inayohusika na kuhudumia shehena ndani na nje ya nchi wakiwa kwenye mahafali ya kumaliza kozi hiyo leo Aprili 6,2023 katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Kaimu Mkeyenge na Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Prof. Zacharia Mganilwa wakiwa katika picha za ya pamoja na wahitimu 22 kutoka nchini Kenya wa kozi ya muda mfupi ya Cargo tallying for international shipping inayohusika na kuhudumia shehena ndani na nje ya nchi.. Hafla ya kuwatunuku vyeti wahitimu hao imefanyika leo Aprili 6,2023 NIT Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad