HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 5, 2023

WAZIRI DKT. PINDI CHANA ATOA RAI KWA WAWEKEZAJI KUWEKEZA KATIKA MICHEZO

  

Na Shamimu Nyaki

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa rai kwa Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika michezo ikiwemo ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya viwanja vya michezo.

Mhe.  Dkt. Pindi Chana ametoa rai hiyo Machi 5, 2023 jijini Arusha wakati wa mbio za Women Fun Run mwaka huu ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 08 mwaka huu.

" Kila Mkoa na Wilaya kuna maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya michezo, nawasisitiza maeneo hayo lazima yalindwe na kutunzwa na kila mkoa wa wilaya lazima utenge maeneo ya kutosha kwa ajili ya shughuli za michezo" amesema Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana.

Mhe. Dkt. Pindi Chana amewasisitiza wananchi waendelee kulinda na kutunza miundombinu ya viwanja vya michezo wanapokua uwanjani kushangilia timu zao.

Mbio hizo za Kilometa 10 na Kilometa 5 zimeratibiwa na Mkoa wa Arusha na kujumuisha Wanawake wa ofisi za Serikali, Sekta binafsi, wafanyabiashara, Wanafunzi na  Wananchi.















No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad