HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 9, 2023

VIONGOZI WANAWAKE WAASWA KUJISAJILI KWENYE KANZIDATA YA TAIFA, SERIKALI YAOMBWA KUTUNGA KANUNI ZA KIJINSIA

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
MBOBEZI wa Hisabati, Profesa Verdiana Masanja ametoa wito kwa wanawake viongozi na wenye fani mbalimbali kuweza kuajiandikisha katika kanzidata ya taifa ya wanawake ijulikanayo kama Women Connect Portal ambayo itasaidia wanawake kujulikana na kuigwa mfano na wasichana wanaochipukia na vizazi vijavyo.

Ametoa wito huo leo Machi 9, 2023 wakati wa Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika Uwanja wa Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa Kanzidata hiyo itatoa hamasa na kuweza kujifunza na kupata hamasa kwa wasichana wanaochipukia kujifunza kutoka kwa wanawake hao.


"Niwatie moyo wadau kuandika simulizi za safari za wanawake, hasa walio katika fani ya teknolojia na sayansi ili kuongeza hamasa kwa watoto wa kike kujiunga na tasnia hii na pia kuelimisha jamii kubadili mitizamo kuwa tasnia hii ni ya wanaume pekee." Amesema


Profesa Verdiana amewapongeza TGNP kwa kuwa kinara katika kutumia teknolojia katika kuimarisha usawa wa kijinsia kwa kutengeneza mifumo mbalimbali, kuwaandaa na kuwahamasisha watoto wa kike kuingia kwenye tasnia ya Sayansi na teknolojia kupitia majukwaa huru na salama ya wanawake pia kwa kujadili changamoto zitokanazo na maendeleo ya teknolojia hususani ukatili wa kijinsia.


Mbobezi huyo wa Hisabati ametambua jitihada zinazofanywa na vyuo vikuu na vyuo vya kati vya humu nchini pamoja na makundi mbalimbali ambao wamekuwa wakihamasisha wanafunzi wa kike kwenye masomo ya sayansi teknolojia uhandisi na hisabati na kushiriki kwenye bunifu mbalimbali ikiwemo na mashindano yanayo andaliwa na wizara ya Elimu sayansi na teknolojia, na Tume ya sayansi na Teknolojia COSTECH.


Amesema kuwa licha ya matokeo chanya ya matumizi ya teknolojia, kuna changamoto zitokanazo na teknolojia. Mfano, wizi kupitia mitandao, ongezeko la ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na utapeli wa kimtandao.


Pia ameipongeza Serikali kwa kuwalinda watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa kutunga sera, sheria ya makosa ya kimtandao (Cybercrime Act 2015), na taratibu ambazo zinawalinda wanawake, watoto na makundi maalum dhidi ya ukatili mitandaoni.


Pia ameiomba Serikali kuimarisha utekelezaji wa sheria zilizopo na itunge kanuni ambazo zitakuwa na mlengo wa kijinsia kwa ajili kutoa ulinzi maalumu kwa watoto wa kike dhidi ya unyanyasaji wa kimtandao.


Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP), Gemma Akilimali amesema sasa kufikiria mikakati madhubuti yenye mlengo wa kijinsia katika kutoa elimu ya masuala ya kidijitali na teknolojia ili kuongeza uelewa kwa wanawake na wasichana juu ya haki na ushiriki katika Maendeleo ya teknolojia ili kuweza kutatua changamoto za kimaendeleo, na kutusaidia kufikia malengo ya endelevu ya dunia.


Amesema elimu ya matumizi sahihi ya teknolojia itasaidia kufika usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu.


Akizungumzia namna ambavyo TGNP wafanya jitihada za kuangalia namna ambazo teknolojia na ubunifu ni kichocheo cha usawa wa kijinsia, amesema maonesho ya teknolojia na ubunifu yatafanyika kwa mlengo wa kijinsia, maonesho hayo yanaoneshwa na TGNP, DIT ili kutatua changamoto za kijinsia na kuwa sehemu ya kuwapa fursa na hamasa wasichana wanafunzi kuweza kufanya vizuri katika eneo hili la sayansi na teknolojia.

Taarifa ya UN Women Gender Snapshots (2022) inaonesha kuwa kutokuwepo kwa wanawake katika ulimwengu wa kidijitali kumepoteza dola za Ukimarekani Trilioni moja katika pato la taifa kwa nchi zenye uchumi wa chini na wa kati kwa muongo uliopita, hasara ambayo inatarajiwa kukuwa hadi kufikia Dola za kimarekani Trilioni 1.5 ifikapo 2025, ikiwa hakuna hatua zitakazochuliwa kuhakikisha ujumuishi wa kundi hili katika masuala ya teknolojia.


Taarifa hiyo imesisitiza kuwa kutokomeza hasara hiyo, nchini hazina budi kuweka nguvu katika kutokomeza ukatili wa kimtandao, ambao utafiti uliofanywa kwa nchi 51, ulionesha kuwa asilimia 38 ya wanawake wamekutana na ukatili huo wao kama wao. Imedhihirika kuwa kuwawezesha wanawake na makundi mengine kushiriki katika eneo la teknolojia ina matokeo chanya hasa katika ubnifu wa suluhisho za changamoto mbalimbali za kijamii na uvumbuzi mwingine unaowasaidia wanawake na watoto wa kike kupata mahitaji yao na hivyo, kuchochea ufikiwaji wa usawa wa kijinsia.


Akiwakaribisha katika warsha ya siku ya wanawake katika Viwanja vya TGNP, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijinsia Tanzania(TGNP), Liliani Liundi amesema isisahaulike kuwa usawa wa kijinsia ni msingi katika kujenga dunia na ulimwengu wa kidigitali salama, jumuishi na wenye usawa kwa wote.


Pia ametoa wito kwa jamii kuchukua hatua zinazowezekana ili kila mmoja ahakikishe teknolojia inatumika kuchochea maendeleo na si vinginevyo.


"Nitoe rai kwa wanawake, wasichana, na wananchi wote wa Tanzania kuendelea kujifunza matumizi sahihi ya teknolojia kuliletea manufaa na maendeleo taifa badala ya kutumia teknolojia, hasa mitandao ya kijamii kufanya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia, nitoe hamasa kwa jamii kutumia teknolojia hii kuelimisha jamii kuachana na vitendo hivyo na kuchukua hatua ili kutokomeza vitendo hivyo.


Wanawake Tanzania kutokupiga picha za utupu wawapo faragha na hivyo kukwepa fedheha pale mambo yanapobadilika. Ombi langu pia kwa watoto wa kike na wanawake wote ni kutokushadadia au kusambaza picha za mwanamke mwenzio kwani kufanya hivyo kunakufanya nawe kuwa sehemu ya ukatili huo. Niwaase pia mabinti zetu na wanawake wenzangu muache kuweka mitandaoni picha za utupu kwani kwa kufanya hivyo pia ni kuchochea ukatili kwa watoto wa kiume na wanaume na kuwapa matamanio yasiyo na ulazima.


Vilevile, unapoweka picha za utupu leo ukumbuke kuwa zitaendelea kukaa huko na ipo siku zitatumika kukuangusha pale unapotafuta fursa au kazi au kujaribu kugombea nafasi ya uongozi. Ni matumaini yangu kuwa tutashiriki kikamilifu katika mijadala mbalimbali ndani ya warsha hii, na kutumia fursa hii kutengeneza na kuimaarisha mitandao na ushirikiano katika kuendeleza na kuimarisha ajenda ya mwanamke na kuhakikisha kuwa warsha hili linaleta mabadiliko katika maisha yetu kama mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla hususani katika matumizi chanya ya teknolojia. "Amesisistiza


Siku ya wanawake duniani hufanyika kila mwaka ifikapo Machi 8. kauli mbiu ya mwaka huu ni "Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia Chachu kuleta Usawa na Kijinsia."
Mbobezi wa Hisabati, Profesa Verdiana Masanja akizungumza wakati wa warsha ya kusheherekea siku ya wanawake dunia ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Machi 8. Pia amehamasisha watoto wa kike kusoma masomo ya Sayansi bila kusahau kujipatia mafunzo ya ukuaji wa teknolojia katika kila nyanja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijinsia Tanzania(TGNP), Liliani Liundi akizungumza wakati wa sherehe za siku ya Wanawake duniani iliyofanyika leo Machi 9, 2023 katika viwanja vya TGN jijini Dar Es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP), Gemma Akilimali  akizungumza wakati wa sherehe za siku ya wanawake duniani iliyofanyik katika viwanja vya TGNP jijini Dar Es Salaam leo Machi 9, 2023.

Wawakilishi  kutoka nchi mbalimbali waliojikita kwenye masuala ya kutetea haki za wanawake na watoto wakizungumza kwa uwakilishi wa nchi zao leo Machi 9, 2023 katika sherehe ya Wanawake iliyofanyika katika Viwanja vya TGNP jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali wakitembelea katika Maonesho ya kisayansi katika viwanja vya TGNP jijini Dar Es Salaam leo.
Picha ya pamoja.
Picha ya Pamoja.

Burudani ikiendelea.

Picha na Avila Kakingo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad